In the News Room
The Web Kilimo web
Home | Budget Speeches | Publications | Agricultural Statistics | Legislations and Regulations | Web Links
 

Waziri  Akutana na Wawezkezaji wa Zao la Miwa

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Prof Jumanne Maghembe amekutana na Bwana Issad Rab Rab kutoka nchini Algeria ambaye pia ni mfanya biashara mkubwa wa mazao yatokanayo na kilimo ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika kilimo cha Miwa, Mpunga, Matunda na Ngano hapa nchini Tanzania.

Mkutano huo umefanyika hivi karibu ofisini kwakena   kumtaka  mwekezaji huyo kuanza kuharakisha mipango yote ya uwekezaji na kuanza kazi hizo mara moja kutokana na mazao wanayotaka kuwekeza kuwa na uhitaji mkubwa hapa nchini na nje za nchi.

“wakulima wetu wanazalisha  kiasi kidogo cha sukari ambacho hakikidhi mahitaji ya watumiaji  hapa nchini, tunaupungufu wa takribani tani nusu millioni za sukari”, alisema Maghembe.

“Hata nchi za jirani kama vile Kenya, Uganda, Somalia na kongo wanahitaji sukari kutoka kwetu, hii ni fursa nzuri kwa kuwa itaongeza uzalishaji wa Sukari ambayo tutaweza kuuza katika nchi hizo”, aliongeza Prof Mahgembe.

Aidha waziri aliongeza kuwa mbali ya kilimo cha miwa , pia zao la mpunga limekuwa likiihitajika kwa upana zaidi Afrika Mashariki na dunian kwa ujumla hivyo kumtaka mwekezaji pia kuangalia uwekezaji katika zao la mpunga hapa nchini.

Alisema Tanzania ipo tayari kuwapatia ardhi katika sehemu tofautitofauti kutokana na kutokuwepo kwa eneo kubwa katika sehemu moja itakayowezesha kulima mazao hayo.

Waziri aliwaomba kushirikiana na wakulima ili waweze kuona faida na matunda ya kutoa ardhi yao kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Bwana Issad Rab alisema endapo watakubaliana wataonza kulima katika msimu ujao ambao unaanza mwezi Novemba mwaka huu, na kuahidi kushirikiana na wakulima kwa kutoa mbegu bora, mbolea na teknolojia za umwagiliaji maji.

Aliongeza kuwa serikali itapata asilimia 40% ya mapato yatokanayo na kilimo hichi pamoja na asilimia 1% kupewa wafanyakazi hodari watakaoshirikiana nao.

Katika kufanikisha swala hilo kwa uharaka zaidi Wazriri Maghembe alisema atakutana na bodi ya sukari na baada ya muda mfupi kwa kushirikiana na na bodi hiyo  watafanya mchakato kubaini sehemem husia.

 

 

 

 

 

 

Uzalishaji wa pamba waongezeka

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Prof. Jumanne Maghembe  Akiongea na wawekezaji kutoka Algeria ambao pia ni wafanya biashara mashuhuri duniani walipomtembelela ofsini kwake

 

Uzalishaji wa zao la pamba nchini, umeongezeka kutoka kilo milioni 168 msimu wa mwaka 2010/11 hadi kufikia kilo million 224 katika msimu wa mwaka 2011/12

Akiongea na wawekezaji kutoka Algeria ambao pia ni wafanya biashara mashuhuri duniani ,  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Prof. Jumanne Maghembe  amesema kuwa katika msimu huu uzalishaji wa pamba umeongezeka kwa kiasi kikukbwa ambacho hakijawahi kutokea  kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita

Aidha Profesa Maghembe aliwaambia wawekezaji hao kuwa moja kati ya mazao ambayo wanaweza kuwekeza hapa nchini ni kilimo cha miwa, ngano matunda  na mpunga, pia aliwataka kuangalia uwezekano wa kuboresha miundombinu ya usafiri wa kutumia bandari ili kuboresha masoko ya mazao kutoka hapa nchini

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Marko Mtunga akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa sekta ya pamba barani Afrika na Ulaya, aliwaambia  ongezeko hilo limechangiwa na serikali kwa kutoa ruzuku za pembejeo.

Mtunga alisema pia ongezeko hilo, limetokana na kuimarika kwa bei ya pamba , kuongezeka kwa mvua na usimamizi mzuri wa zao hilo ambalo ni tegemeo kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Alisema bado uzalishaji kwa heka moja katika maeneo mengi sio mzuri kwa kuwa kuna maeneo yanapata kilo 300 kwa heka na kwamba kwenye maeneo mengine, wanapata kilo 1,000 kwa heka.

Alisema kutopatikana kwa kiasi kikubwa cha pamba katika kila heka kunatokana na kuwapo kwa huduma duni  za maofisa ugani, matumizi duni ya zana za kilimo na pembejeo.

Mkurugenzi huyo alisema pia kuyumba kwa bei ya pamba   ambayo ni kati ya sh 1,100 mpaka sh 800 kwa kilo kunachangia wakulima kutoongeza bidii ya kilimo cha zao hilo.

Alisema Tanzania ina uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha pamba kuliko nchi nyingine zilizopo Kusini na Mashariki mwa Bara la Afrika .

“ Kwa sasa Tanzania inachuana na Zimbabwe katika kuzalisha kiasi kikubwa cha pamba, ’’alisema Mtunga.

Mkurugenzi huyo alisema hivi sasa asilimia 70 ya pamba, inauzwa nje huku viwanda vya ndani vikitumia asilimia 30.

Alipongeza jitihada za jumuiya ya Ulaya, Mfuko wa mazao Duniani (CFC) na wadau wengine  katika kuboresha zao la pamba Barani Afrika.

 

 

 

 

Kamati Yaidhinisha Matumizi ya Aina 26 za Mbegu


Kamati ya Taifa ya mbegu imeidhinisha matumizi ya aina 26 za mbegu mpya za mazao ya kilimo, ambazo zinatarajiwa kuuanza kutumika msimu wa 2012/2013.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika bwana Mohamed Muya alisema hayo jijini Arusha na kueleza kuwa kuidhinishwa kwa aina hizo za mbegu kumetokana na mapendekezo yaliyofanywa na kamati hiyo katika kikao chake kilichofanyika januari 12 na 13 mwaka huu.
 Bwana Muya alisema kamati hiyo imechukua hutua hiyo baada ya utafiti wa kina ambao umewezesha kugundulika kwa aina hizo za mbegu zenye sifa mbalimbali ikiwemo ya kutoa mazao mengi.
Alisema licha ya kutoa mazao mengi sifa nyingine ya mbegu hizo ni kustahimili ukame, ukinzani dhidi ya magojwa, kukomaa mapema na zinapendwa na walaji kwa kuwa zina ladha nzuri.
Katibu Mkuu alisema kati ya aina hizo za mbegu, aina tano ni za kahawa jamii ya Arabika, aina tisa ni za mahindi, aina moja ni ya shayiri, aina nne zao la chai, aina mbili ulezi, aina moja ni ya maharage na aina nne ni za muhogo.
Aliongeza kuwa mbegu hizo zimefanyiwa utafiti wa kina na vituo vya utafiti vya umma na sekta binafsi hapa nchini.Alivitaja vituo vilivyofanya utafiti huo kuwa ni pamoja na Uyole kilichopo mkoani Mbeya, Naliendele kilichopo mkoani Mtwara, Taasisi ya Utafiti wa Zao la Chai (TRIT) ya Iringa, na Taasisi ya  Utafiti wa kahawa (TaCRI) ya Kilimanjaro.
Taasisi binafi zilizofanya utafiti huo ni pamoja na kampuni binafsi za Suba-Agro Trading and Engineering, Pioneer Overseas, Tanzania Breweries, Mansonto na Maru Agro-tours and Consultants.

 

Tumbaku ya Tanzania Kupata Soko Iran

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe  amekutana na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran, Bwana Mohsin Movahhed Ghomi na kumwambia kuwa Tanzania mwaka 2010/2011 ilizalisha kiasi kikubwa cha tumbaku zaidi ya tani 130,000 na kwamba fursa hiyo ya soko ipo nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Iran Bwana Mohsin Movahhed  alisema hiyo ni habari njema kwa viwanda vya sigara vya Tehran na alimuhakikishia Waziri Maghembe kuwa tumbaku hiyo itapata wanunuzi na kuongeza kuwa juhudi zifanyike ili mawasiliano kati ya Ubalozi wake na Serikali ili kuwasiliana na wanunuzi hao ambao wapo tayari kununua kwa kiasi kikubwa

Balozi Mohsin Movahhed aliongeza kuwa Tanzania na Iran zina mahusuano mazuli na ili kuendeleza ushirikiano huo, Iran itaanza kununua mbegu za mafuta kama korosho, karanga na alizeti ambazo nchi hiyo imekuwa ikununua kutoka Pakistan tena kwa bei kubwa wakati inaweza kununua hapa nchini.

Waziri Maghembe alimueleza Balozi Mohsin kuwa Tanzania ina fursa nyingi za kuwekeza hususan katika usindikaji wa bidhaa za mazao ya chakula, mboga na matunda.
“Balozi tunawakaribisha ili muwekeze hapahapa nchi kwa kujenga viwanda vya kusindika korosho kwa kuwa Tanzania ina maeneo ya kutosha na fursa zipo” Alikaririwa Waziri Maghembe.

Naibu Waziri  Aipongeza  ASA

Naibu Waziri wa kilimo Chakula na Ushirika   Christopher Kajolo Chiza (Mb) amezipongeza juhudi zinazofanywa na  ASA katika juhudi za serikali za kuongeza uhakika wa  upatikanaji wa mbegu bora hapa nchini,, kwa lengo la kupunguza utegemezi kutoka nchi zingine. Aliagiza kuza kuwa kuwepo na juhudi za makusudi za kuwashirikisha wakulima wadogo kuzalisha mbegu za kuazimiwa (QDS)

Naibu Waziri vile vile aliwagiza Wahandisi wa Umwagiliaji kufanya uchunguzi (survey) katika mashamba ya Msimba kuhusiana na  ujenzi wa miundombinu ikiwa ni pamoja utokaji wa maji (drainage) kwa lengo la kumwagilia mashamba ya mbegu ili kupunguza utegemezi wa mvua.

Naibu Waziri alimwagiza mchimbaji wa visima kufanya majaribio ya matumizi ya Pampu kutoa maji visimani (pump test) ili kazi zingine zinazohusiana na umwagiliaji zianze mara moja.

Mafunzo kuhusu Mtambo wa Kupokelea Mawasiliano

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Lilian Mapfa jana alifungua rasmi mafunzo ya uelewa kuhusu mtambo wa kupokelea taarifa za hali ya hewa  wa Wizara.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Kitengo cha Mazingira kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)
yana lengo la kuongeza uelewa kuhusu masuala ya taarifa za hali ya hewa ambapo Wizara itakuwa na uwezo wa kutoa taarifa sahihi za kiwango cha mvua kwa wakulima wa Tanzania.

Bibi Lilian alisema  lengo la mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Utalii, Tandika ni kuongeza uwezo wa kufuatilia, kujiweka tayari ili kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira ikiwemo hifadhi endelevu ya mazingira inayochangia kupunguza umaskini.

Bibi Mapfa aliongeza kuwa mtambo huu utasaidia kufanikisha shughuli za kilimo, utafiti katika kilimo hasa mbegu.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mazingira cha Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Shekwanande Natai alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia Wataalam wa Wizara kujua namna ya kutumia mtambo huo na faida zake.

Wahandisi Umwagiliaji,  Wasaidie  Kuibua Miradi ya Umwagiliaji

Naibu Waziri wa Kilimo chakula na Ushirika Mhe. Christopher Kajolo Chiza amewagiza Wahandisi wa Umwagiliaji,  Kuwawezeshe wakulima kuibua miradi ya umwagiliaji.

Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya Wahandisi wa Umwagiliaji wa Umwagiliaji wa Kanda, Sekretariati za Mikoa na Halmashauri za wilaya, yaliyofanyika mjini Morogoro hivi karibuni

Mhe. Chiza aliagiza kuwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya  miradi ya umwagiliaji lazima zitumike kama zilivyokusudiwa.

Alisisitiza kuwa  wakulima wajulishwe  kiasi cha fedha kinachotumika katika miradi ya umwagiliaji, maana ya mifuko (Vyanzo vya  fedha)  ikiwa ni pamoja na umoja wao unaowawezesha kutekeleza vizuri miradi ya umwagiliaji.

Aidha Mhe. Chiza alisema kuwa serikali inalenga kuwa ifikapo mwaka 2015 asilimia 25 ya chakula chote kinachozalishwa nchini kitokane na  kilimo cha Umwagiliaji, kwa kuongeza maeneo ya kilimo hicho kufikia hekta 1,000,000, na vile vile kulima kisasa katika maeneo yalioyopo

Kituo cha Technolojia ya Kuendeleza Kilimo Chafunguliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Jakaya Kikwete amefungua kituo cha teknolojia ya kuendeleza kilimo kilichojengwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China katika Kijiji cha Cholima, Dakawa, Wilayani Mvomero katika mkoa wa Morogoro.
Kituo hicho kina ukubwa wa ekari 62 kilijengwa kufuatia ziara ya Rais Kikwete nchini China ambapo serikali ya China ilikubali kujenga kituo hiko ikiwa ni mojawapo ya Vituo 14 vitakavyojenga barani Afrika katika kusaidia sekta ya kilimo.

Awali akizungumza juu ya Kituo hicho, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Profesa Jumanne Maghembe alianza kwa kumshukuru mheshimiwa Rais

kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo.
Mheshimiwa Waziri alibainisha kuwa kituo hicho cha kuendeleza teknolijia ya kilimo ni matokea ya mkutano uliofanyika nchini China baina ya viongozi wa Afrika na Serikali hiyo. Na katika mkutano huo Serikali ya China ilikubali kujenga vituo 20 vya kuendeleza kilimo katika Bara la Afrika.
“Ujumbe wa wataalam kutoka China ulitembelea Tanzania mwaka 2008 na kuweka saini makubaliano ya ujenzi wa kituo hicho na baada ya kuweka saini hiyo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitenga eneo kwa ajili ya mradi huo ambapo mwezi Oktoba 2009 ujenzi ulianza na kukamilika baada ya miezi 13” aliongeza Waziri.
Ujenzi na gharama ya vifaa katika kituo hiki umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.8 za Kitanzania huku shughuli muhimu zitakazokuwa zikifanywa na kituo hicho zikiwa ni pamoja na kufanya majaribio kwa mbegu mpya za mazao mbalimbali, kufanya utafiti na kufanya maonyesho ambayo yatawafanya wakulima kujifunza namna ya kukuza mazao mbalimbali, kuendeleza mifugo kama kuku na kuimarisha mashamba yao kwa kupambana na visumbufu vya mazao na kadhalika alikaririwa Profesa Maghembe.
“Aidha Kituo kitaendesha mafunzo ya muda mfupi na semina kwa Wagani na wakulima kuhusu teknolojia za kisasa katika kilimo kwani ni kituo kikubwa kabisa nchini kwetu Tanzania na kimekuja wakati muafaka na kwamba nchi yetu inatekeleza miradi mbalimbali ya kilimo kupitia programu ya ASDP na Azimio la KILIMO KWANZA” alisema Mheshimiwa Maghembe

Kwa upande wake Rais Kikwete aliagiza Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika chini ya Waziri Maghembe kuhakikisha inasimamia kituo hicho kwa manufaa ya taifa na kuhakikisha hakifi baada ya waliokijenga kuondoka ndani ya miaka mitatu ijayo.

 

Kamati ya Bunge Yatoa ushauri Kwa Wizara

Kamati ya Bunge iliyotembelea Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) hivi karibuni wameishauri Serikali kuongeza juhudi katika kusambaza chakula cha msaada kwa waathirika wa njaa katika Wilaya na Halmashauri zilizokumbwa na tatizo hilo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Wajumbe wa Kamati hiyo wamesema kuwa inachukua muda mrefu kwa chakula cha msaada kuwafikia walengwa kwa sababu ya kuwepo kwa kamati nyingi za ugawaji wa chakula hicho hivyo kuzidi kuwapa hali ngumu walengwa.
Aidha Wajumbe wa Kamati hiyo wamesistizia Idara ya Usalama wa Chakula kutoa ushirikiano mkubwa  kwa  Halmashauri wakati wanapofanya tathimni ili kupata Idadi kamili ya waathirika wa njaa na kuepuka taarifa zisizo sahihi.
Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Kilimo Chakaula na Ushirika  Bibi Sophia Kaduma aliieleza Kamati ya Bunge ya Kilimo Maji na Mifugo kuwa  changamoto kubwa kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ni upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia nafaka na idadi ndogo ya maghala.
Alibainisha kuwa kiwanda kinachozalisha magunia ya katani hapa nchini hakina uwezo wa kutosha wa kuzalisha, hivyo kushindwa kusambaza magunia katika taasisi za Wizara ya Kilimo hasa ikizingatiwa kuwa Wizara ina uhitaji mkubwa wa magunia ya kuhifadhia kahawa, pamba na mazao mengineyo katika tasisi zake.
Kuhusu uhaba wa chakula Bibi Sophia Kaduma  amesema kuwa tathimini hufanywa  mapema pindi taarifa zinapopatikana kutoka katika vyanzo  husika.

Wilaya ambazo zimepata upungufu wa chakula zimeshafanyiwa kazi na Wilaya nyingine zilizojitokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashugulikiwa haraka alisema Naibu Katibu Mkuu.
Upungufu wa Magala ni changamoto nyingine inayoikabili Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirka ambapo, Wizara ina uwezo wa kuhifadhi Tani Laki Mbili na Elifu Arobaini na Moja tu (241,000) katika maghala yote ingawa lengo ni kuwa na uwezo wa kuhifadhi Tani Laki Nne alisema Naibu Katibu Mkuu

 

Waziri Azungumza na Watumishi wa Makao Makuu

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Profesa Jumanne Maghembe  amekutana na watumishi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Makao Mkuu na kujadili mambo mbalimbali.

 Katika Mkutano huo Waziri Maghembe alianza kwa kuwapongeza Watumishi wote kwa juhudi zao katika utendaji wa kazi za kila siku.

Kabla ya kusikiliza mawazo na michango ya Watumishi alisema kuwa ni lazima Watumishi waamue kwa makusudi kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kumuongezea kipato mkulima wa Tanzania.

Waziri Maghembe aliongeza kuwa ni vyema kama Taifa kuitumia fursa ya kupanda kwa bei ya mazao ya biasha ra kwenye soko la dunia na kutoa mfano wa bei ya pamba imepanda na kufikia shilingi  800 kwa kilo tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ilikuwa ni shilingi 350.

alisema katika shughuli za kilimo kumekuwa na changamoto nyingi zikiwemo za  wakulima kutotumia mbolea, wadudu na wanyama waharibifu pamoja na elimu duni na matumizi finyu ya mbegu bora kwa wakulima.
“Kama wagani wataweza kufanya kazi yao vizuri  na wakulima wakapata ujumbe wetu vizuri na tukawapatia soko la bidhaa zao basi tutazalisha  zaidi ya asilimia 6” alikaririwa Waziri Magheme.
Hata hivyo Waziri alisisitiza kuwa ili kilimo kiwe na mafanikio ni lazima mbegu bora zizalishwe hapa…..

nchini hasa kwa kuzingatia mazingira husika ili  kuepusha hasara kwa kuwa mbegu za ndani zinakuwa na sifa ya hali ya hewa ya hapa nchini na kuwa na ukinzani dhidi ya magonjwa tofauti na zile zinazozalisha nje ya nchi.

Aidha Waziri Maghembe alisisitiza kuongezwa kwa eneo la kilimo cha umwagiliaji maji mashamba ambacho kina uhakika zaidi ya kilimo cha kutegemea mvua.

 

 

Japani Kuendeleza Kilimo cha Mpunga Nchini

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Jumanne Maghembe na Balozi wa Japan Bwana Hiroshima Nakagawa

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe  na Balozi wa Japan  nchini Bw. Hiroshi Nakagawa, wamekutana na kuzungumzia uwezekano wa Japan, kushirikiana na Tanzania  katika kuendeleza zao la mpunga kwa kuleta wataalam wa umwagiliaji ili waweze kutoa mafunzo na elimu wakishirikiana na wenzao wa hapa nchini.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amefanya mkutano huo na Balozi Hiroshi Nakagawa ofisini kwake hivi karibuni.

Katika mkutano huo  Waziri  alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi Hiroshi Nakagawa wa Japan kwa ushirikiano mkubwa uliopo baina ya nchi hizi mbili katika masuala mbalimbali hasusan Kilimo.
Aidha Waziri Maghembe alimueleza Balozi Nakagawa kuwa ushirirkiano huo unalenga  kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji maji mashamba na barabara ili kuimarisha uzalishaji wa zao la mpunga nchini kwa lengo la kumuongezea mkulima kipato.

Pamoja na hayo Waziri Maghembe alisema maeneo ya  ushirikiano ni pamoja na kuandaa wataalam wa umwagiliaji maji mashamba ili kutumia rasilimali zilizopo.
Waziri Maghembe aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika ambayo ina maji mengi ambayo hayajatumika, hivyo Japan itashirikiana na Tanzania

katika umwagiliaji maji mashamba kwa kutoa mafunzo kwa wataalam na wakulima  ni dhahiri kuwa Taifa litapiga hatua kwa kiasi kikubwa alisema Prof . Maghembe.
 
Naye Balozi Nakagawa alisema kuwa Japan ilishaanza kutoa mafunzo ya umwagiliaji katika Chuo cha Kilimo cha KATC kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo katika ushirikiano huo mbinu hizo zitatumika katika kuwafikia wakulima

 

 

 

SERIJALI YAJIPANGA KUJENGA KIWADA CHA KUBAGUA KOROSHO

Naibu Waziri wa kilimo chakula na ushirika Mh. Chiristopher Chiza amekutana na  wawekezaji wa korosho  kutoka katika taasisi mbalimbali za Maerekani (AFRICA HARVEST OF HOPE)’kujadili uwezekano wa kujenga  kiwanda cha kubangua korosho hapa nchini.
 
Akizungumza na wawekezaji hao amesema kuwa  Serikali ya Tanzania inalikaribisha wazo la kujenga kiwanda cha kubangua korosho   kwa lengo la kuongeza ubora wa zao la korosho ili liweze kupata soko zuri hapa nchini na nje ya nchi.

Aidha Mhe. Naibu Waziri  alisema kuwa, mkulima anapata hasara kwa kuuza korosho gafi hivyo kumfanya apate hasara na kushindwa kuondokana na umaskini.

Katika uwekezaji huo Naibu waziri amewataka  wawekezaji hao  kufanya mabo yafuatayo ili kukamilisha tarabu za uwekezaji, kwanza wakitembelee kituo cha uwekezaji (Tanzania Investment Centre), kwa ajili ya kupata mwongozo wa uwekezaji.

Pia wawekezaji hao wawe tayari kuwashirikisha wakulima katika shughuli zao na wawe tayari kuwa na kilimo cha  mkataba  kitakachomwezesha mkulima kuwa na  uhakika wa kipato chake.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Bw. Patrick Chiles alisema kuwa, mradi wao ‘AFRICA HARVEST OF HOPE’ unakusudia kwekeza Tanzania katika zao la korosho, baada ya kuona kuwa zao hili linazalishwa  Tanzania lakini sehemu kubwa inasindikwa  nchini India na kuuzwa nchi zingine, hivyo wameona ni vizuri korosho isindikwe hapa hapa Nchini.

Walitoa ahadi kwamba watafuata taratibu zote za uwekezaji,, kununua korosho nyingi kwa ajili ya kuongeza ajira  ya muda mrefu, ambapo wamesma wamesea pia kuwa  Taasisi yao haitakuwa ya kutengeneza faida kubwa.

 

DRD Yadhamaria Kusajili Watafiti

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Fidelis  Myaka

 

Idara ya Utafiti na Maendeleo imedhamiria kuweka mkakati wa kuwasajili watengeneza mbegu (Breeders) ili kuwabana wale ambao hawana sifa kama njia ya kuboresha upatikanaji wa mbegu bora.

Azimio hilo lilifikiwa na Wajumbe wa Mkutano wa Kitaifa wa Utafiti wa mbegu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  Hoteli ya Safari uliopo mjini Arusha hivi karibuni.

Katika Mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Fidelis Myaka pamoja na Watafiti wengine, wamedhamiria kuanzisha mkakati wa usajili wa wazalisha mbegu baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wakulima na baadhi ya Kampuni za kuzalisha mbegu walidai kuwapo mbegu ambazo  zina kiwango duni na kukosa sifa kadhaa.

Katika usajili huo utaonyesha viwango   vya kitaaluma anavyotakiwa kuwa navyo mzalishaji wa mbegu na  aina za mazao ambazo  anatafiti.

Dkt. Myaka aliendela kusema kuwa Idara itafanya ukaguzi wa Taasisi za utafiti kubaini kama kuna aina za watafiti wasiokidhi viwango ikiwa ni jitihada za kuimarisha uzalishaji wa mbegu. “Kwa kufanya hivi itasaidia kuwarekebisha baadhi ya  Watafiti ambao wanataaluma tofauti na  mbegu wanazozizalisha alisema Dkt. Myaka.

Naye Mwenyekiti wa Mkutano huo Bwana Geoffrey Kirenga amesema Usajili huo utamuweka huru mzalishaji mbegu atakayeamua kuzalisha mbegu tofauti na fani yake kusomea ili kupata taaluma husika, aliongeza kuwa kuwasajili wazalisha mbegu kutaliwezesha taifa kuzalisha mbegu zenye ubora na hatmae kuchangia katika kuinua kilimo alisisitizwa, Bwana Kirenga

 

Jumuia ya Ulaya Kuendelea Kusaidia Sekta ya Kilimo

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Jumuia ya Ulaya, Bwana Tim Clarke ofisini kwake

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa, Profesa Jumanne Maghembe amekutana na Balozi wa Jumuia ya Ulaya, Bwana Tim Clarke ofisini kwake hivi karibuni na kuzungumza masuala yanayohusu sekta ya kilimo nchini na namna ya kudumisha na kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Jumuia ya Ulaya.

      Balozi Clarke alimueleza Waziri Maghembe kuwa Jumuiya ya Ulaya imedhamiria kuendeleza zao la kahawa na mazao mengine kupitia programu mbalimbali zinazotekelezwa na Jumuia ya Ulaya Barani Afrika.

   Balozi Clarke aliainisha miradi ambayo Jumuiya hiyo inatilia mkazo kuwa ni pamoja na ule wa kuendeleza kilimo cha miwa uliogharimu Euro milioni 6, Progarmu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo, ASDP Euro Milioni 32, utafiti wa zao la chai, Euro milioni 2 na Utafiti kwa kahawa Euro milioni 2.

    Balozi Clarke aliongeza kuwa Euro milioni 30 zipo tayari kusubiri utekelezaji na kuongeza kuwa Jumuia hiyo imeisaidia Tanzania kiasi cha Euro milioni 50 zilizowekezwa kwenye kilimo tu.

     “Jumuia ya Ulaya imetenga Euro bilioni 1 kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa chakula barani Afrika na katika mgao huo Tanzania itapata Euro milioni 32” alikaririwa Balozi Clarke.

    Balozi Clarke aliongeza kuwa Jumuia ya Ulaya inafadhiri  miradi nane nchini ukiwemo ule wa Tanzania Agricultural Partnership – TAP ambao utatekelezwa kati ya Serikali  na Jumuia hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuangalia eneo la usalama wa chakula, virutubisho (nutritions) na  kujenga uwezo wa wataalam katika  Vyuo vya Mafunzo kama vile Tengeru alisema mwakilishi huyo wa Jumuia ya Ulaya.

   Kwa upande wake Waziri Maghembe alimueleza mwakilishi huyo nia ya Serikali katika kuhakikisha  kilimo cha Tanzania kinakuwa cha kisasa, chenye tija na enedelevu kinacholenga  kubadili maisha ya wakulima wadogo na wakubwa na kukuza uchumi wa Taifa kwani asilimia 85 ya Watanzania wanajihusisha na kilimo.


 

 

Naibu Waziri atembelea Mkoa wa kigoma

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Chiza akitoa maelekezo kwa mafisa wa wilaya ya Kibondo

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Chiza  hivi karibuni alimaliza ziara ya kikazi ya  siku sita katika  Mkoa wa Kigoma katika Wilaya za Kigoma Vijijini, Kibondo,na Wilaya mpya ya Kakonko.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri alifanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa usambazaji pembejeo  ya ruzuku ikiwa ni pamoja  na kupata maelezo na changamoto zilizojitokeza katika utaratibu mzima wa usambazaji wa pembejeo hizo. Moja ya changamoto kubwa iliyoelezwa na baadhi ya wakulima, ni kwa wakulima  kuweka sahihi kwenye vocha bila ya kuchukua  pembejeo husika kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulipia  pembejeo zikiwemo mbegu bora na mbolea

Aidha Mhe. Eng. Chiza aliuagiza  uongozi wa wilaya husika  kufanya ufuatiliaji wa karibu katika zoezi  zima la usambazaji wa pembejeo ili kubaini baadhi ya mawakala ambao sio waaminifu. Katika ufuatiliaji huo kila mkulima aliyeweka saini kwenye vocha itabidi athibitishe kuwa alipokea  pembejeo, na kasha kuonyesha shamba lake zilipotumika  pembejeo hizo.

Mhe Eng. Chiza  vile vile alipata fursa  ya kutembelea wakulima wa zao la kahawa katika kijiji cha Muhange , Shughuli za kilimo cha umwagiliaji na katika kijiji cha Nyamtukuza na Kituo  cha mpakani cha Mabamba katika wilaya ya Kibondo kinachoshughulikia  Ukaguzi wa Mazao na Afya ya Mimea.  

 

 

Tanzania na Israel Kuendeleza Mahusiano

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Mohamed Muya na Balozi wa Israel Afrika ya Mashariki, Bwana Jacob Keidar ofisini kwake hivi karibuni

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bwana Mohamed Muya amesema nia ya Serikali ni kukuza na kuboresha kilimo ili sekta hiyo iwe ya manufaa Kitaifa na Kimataifa.

Akizungumza na Balozi wa Israel wa Afrika ya Mashariki Bwana Jacob Keidar ofisini kwake hivi karibuni, Bwana Muya alisema kilimo kitaboreshwa kwa mikakati mbalimbali kama Kauli Mbiu ya KILIMO KWANZA na Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia fursa za Tanzania unaojulikana kama (Southern Agricultural Corridor of Tanzania - SAGCOT) ambao ilizunduliwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa, Mizengo Pinda wiki mbili zilizopita.
Aliongeza kuwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika inatekeleza programu ya ASDP (Agricultural  Sector Development Program)

Akizungumzia Azimio la KILIMO KWANZA,  Bwana Muya alisema Kauli Mbiu hiyo ina dhamira ya kubadili kilimo kutoka kilimo cha kujikimu na  kuwa cha kisasa na cha kibiashara kwa kushirikiana na sekta binafsi ili isaidie kuwekeza hasusan kwenye upatikanaji wa mbegu bora za kilimo na si kuiachia Serikali peke yake.

Aliongeza kuwa mahitaji ya mbegu kwa wakulima wa Tanzania ni tani 120,000 kwa mwaka na uwezo wa ndani wa kuzalisha mbegu ni jumla ya tani 6,000 tu ambazo hazitoshelezi.

“Kwa sasa tuna uwezo wa kuzalisha tani 6,000 tu za mbegu bora ambazo hazitoshi kwani mahitaji halisi kwa mwaka ni tani 120,000”. Alikaririwa Bwana Muya.

      Katibu Mkuu alieleza nia ya kuboresha sekta ya kilimo kwa kupitia kilimo cha umwagiliaji na kuhama kutoka matumizi ya jembe la mkono ambalo linatumia muda mwingi na uzalishaji mdogo na kuboresha miundombinu kama barabara ili kuwawezesha wakulima kusafirisha na kuuza mazao yao kwa urahisi.

     Naye Meneja wa Kampuni ya  Balton, Tanzania Bwana Ilan Hanegbi alisema, Kampuni hiyo imejikita zaidi kwenye uuzaji wa miundombinu na mitambo ya kilimo cha umwagiliaji maji mashamba hususan umwagiliaji wa matone (Drip irrigation).
 
    Aliongeza kuwa Kampuni hiyo imewekeza katika Mikoa kadhaa nchini kwa lengo la kuhamasisha kilimo cha umwagiliaji maji mashamba kwa wakulima wadogo na wakubwa. Aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni Dodoma (Chilangali SACCOS) na Kilimanjaro (Miwaleni- Moshi) ambapo ufanisi umeanza kuonekana. 
  
    Bwana Hanegbi alisema Balton ipo tayari kugharamia na kuwasomesha wakulima wadogo kupitia ofisi zao za Mikoani ili wapate elimu ya umwagiliaji maji mashamba na elimu ya uhifadhi wa mazao mara baada ya kuvunwa.

Marekani  Kuisaidia Tanzania Katika Sekta  ya Kilimo

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiwa na Balozi wa Marekani nchini, Bwana Alfonso Lenhardt (kulia)

Marekani imeahidi kuendelea  kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali hususan Kilimo. Hayo yemesemwa na Balozi wa Marekani nchini, Bwana Alfonso Lenhardt alipokutana na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe jana akiambatana na ujumbe maalum kutoka Marekani.
Balozi Alfonso Lenhardt alimueleza Waziri Maghembe kuhusu mradi wa “FEED THE FUTURE” kwa kusema kuwa sasa ni wakati muafaka kwa mradi huo kuanza kutekelezwa nchini kwa kuwa una faida kubwa kwa taifa, Balozi Alfonso alizitaja nchi nyingine zilizo katika mradi huo kuwa ni Salvado, Philipines na Ghana.
“Tanzania imechaguliwa kutokana na hatua kubwa iliyopiga katika sekta ya kilimo na dhamira yake ya dhati katika kutekeleza
usalama wa chakula, virutubisho vya mazao na ongezeko la uzalishaji”. Balozi Alfonso Lenhardt  alisema, katika mkutano wa Milenia Rais Obama aliitolea mfano Tanzania kama nchi inayotambulika na Marekani kwa kuonesha kwa nadharia na vitendo jinsi ilivyodhamiria kuendeleza kilimo nchini. Vilevile nchi ya Marekani kutoka kwenye mradi wake wa Millennium Challenge Compact imetenga Dola milioni 600 kwa Tanzania maalum
kwa ujenzi wa barabara na miundo mbinu mingine ili kusaidia sekta ya kilimo kukua na kupanuka kwa haraka. “FEED THE FUTURE inalenga kuwaunganisha Wakulima kwa kutumia miundombinu mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi jirani kwa lengo la kupata masoko” aliongeza Balozi Alfonso.
Mradi huo wa FEED THE FUTURE pia utasaidia katika maeneo mbalimbali kama vile matumizi bora ya ardhi, kusaidia wakulima wadogo na usafirishaji wa mazao. Kadhalika, nafasi ya mwanamke itawekewa mkazo sambamba na  mipango maalum ili Tanzania iweze kufikia malengo yake katika Kilimo.
FEED THE FUTURE utalenga katika kusaidia mazao ya mpunga, mahindi na mazao ya bustani. Katika mkoa wa Arusha kumekuwa na maendeleo makubwa kwa mazao hayo hivyo kuifanya Serikali ya Marekani kuzidi kusaidia Tanzania na watu wake. Mojawapo ya mradi wa barabara mkubwa ni ule wa kutoka Tunduma mpaka Sumbawanga. Miradi ya umwagiliaji ni pamoja na skimu 7 zilizo mkoani Morogoro.
Kwa upande wake Waziri Maghembe alichukua fursa hiyo kuishukuru Marekani kupitia Balozi na ujumbe wake na kuahidi ushirikiano madhubuti baina ya nchi hizo mbili. Vilevile Waziri Maghembe alizungumzia jinsi ya kuongeza fursa zaidi baina ya nchi hizi mbili katika soko la mazao ya kilimo.

     
Speeches| Publications | Agricultural Statistics | Legislation and Regulations | About us|Contact us
Copyright 2008, Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives All rights reserved.