Home Up Feedback Search

Inputs
Home Up

Soma kipeperushi cha kuhusu mikopo ya pembejeo

       

United Republic of Tanzania, Ministry of Agriculture, Food Security & Corperatives, Agricultural Inputs Trust Fund. AGITF.  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mfuko wa Pembejeo.

Taratibu na Masharti ya Mikopo ya Pembejeo za Kilimo na Mifugo

  1. Waombaji wa mikopo ya pembejeo watatakiwa kujaza fomu maalim za maombi zinazopatikana kwenye Halmashauri za Wilaya husika. Afisa kilimo wa Wilaya husika atathibitisha shughuli za mwombaji pamoja na vielelezo vinavyohitajika kabia ya kuzipitisha.  Fomu   zilizokamilika   na kupiitshwa na Afisa Kilimo wa Wilaya, zitaidhinishwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya kabia ya kutumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
    Pembejeo. Ili maombi haya yashughulikiwe ipasavyo inashauriwa yawasilishwe mapema
    katika muda maalum kama ifuatavyo:-
    bullet

    Maombi kutoka mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Kigoma, Kagera, Mara na Mwanza yatumwe kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Pembejeo katika kipindi cha kati ya mwezi Machi
    hadi Juni.

    bullet

    Maombi kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro,Mtwara, Lindi na Dar es salaam yatumwe kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Pembejeo katika kipindi cha kati ya mwezi Julai hadi Septemba.

  2. Maombi ya wauza pembejeo binafsi, wakulima na wafugaji binafsi sharti watimize masharti yafuatayo:-

 

bullet

Wawe    na    dhamana    binafsi isiyohamishika yenye hati miliki (title deed) na inayokubalika kisheria.

bullet

Watatakiwa kutekeleza masharti ya mikopo ya benki au taasisi nyingine ya kifedha itakayotoa mikopo kwa niaba ya Mfuko wa Pembejeo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti na benki husika na
kulipa asitimia moja ("1%) ya mkopo
kabia  mkopo  haujaidhinishwa  na
kutolewa.

  1. Maombi ya Mifuko ya Pembejeo ya Wilaya isiyo na dhamana zenye hati miliki sharti idhaminiwe na Halmashauri za Wilaya husika.

  2. Maombi ya Vyama vya kuweka na kukop (SACCOS), vikundi vya wakulima na wafugaji visivyo na dhamana za hati miliki sharti viwe wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa Tanzania (SCCULT, 1992 Ltd.). Kiasi cha mkopo utakaotolewa ni mara tatu ya akiba ya mwombaji itakayowekwa SCCULT, (1992) Ltd. kama dhamana.

 

Send mail to agitf@mari.or.tz with questions or comments about this web site.
Last modified: 03/06/07