1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana
katika Ofisi za kilimo za Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa
Pembejeo, jijini Dar-es-salaam na katika tovuti yetu.
2. Fomu za maombi zilizojazwa na kuambatanishwa na
vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa Kilimo wa
Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika na
baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.
3. 3. Mikopo ya kununua matrekta inapitia benki, mwombaji sharti
atimize yafuatayo:-
-
Awe na dhamana
binafsi kwa jina lake isiyohamishika yenye hati rriliki (title deed) na inayokubalika kisheria.
-
Awe tayari kutekeleza
masharti ya mikopo ya benki itakayotoa mikopo kwa niaba ya Mfuko wa
Pembejeo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti na benki husika, kulipa
asilimia moja ya mkopo kabla haujatolewa na kusajili trekta kwa jina lake
na benki au taasisi ya fedha itakayotoa mkopo.
-
Awe tayari kulifanyia
matengenezo madogo na makubwa trekta litakalonunuliwa kwa
mkopo mara kwa mara kama atakavyoelekezwa na mtengenezaji au muuzaji wa
trekta hilo.
4. Muda wa mkopo ni miaka mitatu kwa riba ya asilimia kumi
(10%)