1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana
katika Ofisi za kilimo za Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa
Pembejeo, jijini Dar-es-salaam na katika tovuti yetu.
2. Fomu za maombi zilizojazwa na kuambatanishwa na
vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa Kilimo wa
Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika na
baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.
3. 3.
Mikopo ya kununua matrekta
inatolewa na Mfuko wa Pembejeo, baadhi ya benki na taasisi za fedha na
SCCULT (T) Ltd. kwa niaba ya Mfuko, mwombaji sharti
atimize yafuatayo:-
-
Awe na dhamana yenye hati
miliki isiyohamishika iliyoandikishwa kwa jina la mwombaji.
-
Awe na shamba binafsi lisilopungua hekta 50 na awe tayari kutoa huduma ya kuwalimia wakulima
wengine
-
Awe tayari kutekeleza
masharti yote ya Mfuko wa Pembejeo au taasisi ya fedha na SCCULT
yanayohusu mkopo wa ununuzi wa trekta jipya.
-
Awe tayari kulipa asilimia
moja (1%) ya mkopo kama gharama za nyaraka za mkopo na kusajili trekta kwa pamoja kwa
jina lake na Mfuko
-
Riba inayotozwa ni
asilimia nane (8%) na marejesho hufanyika kwa muda wa miaka mitatu kila
baada ya miezi mitatu.