Mhe. Bashungwa. Ateta na Wanaushirika

Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa  amesema mfumo wa ushirika  ni nyenzo muhimu ambayo ukitumika vizuri itasaidia kuondoa  umaskini wa wakulima hapa nchini na utaimarisha uanzishwaji wa viwanda kuleta tija katika kilimo.

Akiongea leo katika mkutano na menejimemnti ya Tume ya Ushirika katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa kilimo VI amesema ushirika lazima uwajengee  uwezo wakulima ili kupata faida kwenye mazao yao.

Aidha amewataka wanaushirika kote nchini kuwa na mipango kazi ambayo itasaidia kufanya kazi zao za kila siku ambapo itasaidia kufikisha malengo ya nchi  na itaondoa migogoro na migongano katika vyama vya ushirika.

Bado ushirka haujawasaidia sana wakulima bado wakulima wanauza bidhaa zao kwa bei ya chini sana ni lazima tufufue ushirika  kwa nguvu zote ili  mabailiko wa sekta ya kilimo yaletwe na ushirika, Ni lazima ushirika utumike kuwajengea uwezo wakulima na kuleta matokeo makubwa kwa wananchi  alisema Mhe. Bashungwa.

Hata hivyo amewataka wanaushirika kuendelea kutoa elimu kwa vijana ,wanawake  na vikundi vyenye  mwelekeo  wa ushirika  na  wakulima kwa ujumla kuhusu umuhimu wa ushirika kuliko kuwa navitu vizuri ambavyo vinabaki kwenye makaratasi  alisistiza Mhe. Bashungwa.

Awali Naibu Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bwana Charles Malunde amesema ushirika unakabiliwa na changamoto ya masoko endelevu kwa mazao na bidhaa za wanaushirika.

Aidha Bwana Malunde amesema tayari tume ya ushirika imeanza  kushirikiana na taasisi zote zinazojihughulishaa  na uwekezaji ili kupata  masoko ya mazao  na bidhaa mbalimbali za wanaushirika

Ukosefu wa mfumo wa TEHAMA  kwa  ajili ya usimamizi wa utendaji wa vyama vya ushirika  umekuwa ni changamoto kubwa katika kufanikisha shughuli hizo alimalizia Bwana Malunde.

Naye Kaim Mkurugenzi wa  Kitengo cha Utafiti   na Elimu Bi Doroth Kalikamo kutoka Tume ya Ushirika amesema utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonesha kwamba ili ushirika uweze kushamiri ni lazima ufundishwe katika ngazi zote za elimu ikiwemo vyuo vya ufundi VETA ili uweze kutoa hamasa kwa wanachi.

Hata hivyo Bi Doroth alimalizia kwamba ushirika ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania hivyo ni vizuri kuwe na data zitakazo onesha mchango wake katika uchumi wa taifa kwa mwaka.