Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Yakabidhiwa Gari la Sh 88 Milioni

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bi. Nkuvililwa SimkangaKaimu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bi. Nkuvililwa Simkanga

Taasisi ya Ushirikiano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) imeikabidhi Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi gari lenye thamani ya shilingi milioni 88 za kitanzania itakayotumika katika Idara ya Mipango na Sera.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bi. Nkuvililwa Simkanga ndiye aliyepokea gari hilo katika hafla iliyofanyika katika viunga vya wizara hiyo.

Gari hilo litatumika katika Mradi wa Micro Reform for African Agribusiness Project (MIRA) ambao ni mradi wa kufanya mageuzi ya kisera na kisheria yanayokwamisha utekelezaji wa sekta binafsi katika kilimo unaosimamiwa na Idara ya Mipango na Sera.

MIRA ni mradi utakaogharamiwa na AGRA na utekelezaji wake utaratibiwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

“AGRA ni wadau wetu wakubwa na wamekuwa pamoja na Wizara bega kwa bega katika kuinua kilimo chetu kwa nguvu zote” aliongeza Bi. Simkanga.

Bi. Simkanga aliishukuru sana AGRA kwa kuendelea kushirikiana na Wizara katika kundeleza kilimo hapa nchini.

Mradi huu unategemea kutekelezwa kwa muda wa miaka 5 kwa kiasi cha Dola za Marekani zipatazo milioni 50 na umeanza kutekelezwa tangia Juni 2015 na utafikia kikomo Juni 2019.

Mbali ya gari vifaa vingine vilivyokabidhiwa hapo awali kuwa ni Komputa Mpakato (Laptop) na flash na hii ni kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Bw. Gungu Mibavu.

Naye mwakilishi wa AGRA Bw. Vianey Rweyendela amepongeza ushirikiano uliopo kati ya AGRA na Wizara katika harakati za kuinua kilimo na akasisitiza kuwa kupitia ushirikiano huu vitafanyika vitu ambavyo havijafanywa katika kuhakikisha kuwa kilimo kinasonga mbele.

“Tumedhamilia kuhakikisha kuwa partnership yetu tunafanya vitu ambavyo havijafanywa katika Sekta ya Kilimo hapa nchini” alisisitiza Bw. Rweyendela.

Wawakilishi wengine katika hafla hiyo alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango toka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Gungu Mibavu na Liston Njoroge toka AGRA.