HOTUBA YA KUKABIDHI MATREKTA KWA
28 SEPTEMBA, 2004
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Ndugu Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana
Napenda
kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Mkoa na wa
Tanzania Cotton association kwa Mapokezi tuliyopata tangu tulipowasili katika
Mkoa wa Mwanza. Ninapenda kutoa shukrani
za pekee kwa Tanzania Cotton Association kwa kunialika kuwa mgeni rasmi
katika sherehe hii ya kukabidhi matrekta kwa wanachama wenu. Nawapongeza kwa kazi hii nzuri mliyofanya.
2. Ndugu Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hii kutoa pongeza kwa Tanzania Cotton Assosication, kwa juhudi mnazofanya za kuendeleza kilimo cha kutumia zana bora za kisasa. Nina taarifa kuwa baadhi yenu mmekuwa mkitoa pembejeo na kuwalimia mashamba wakulima wanaozunguka vinu vyenu vya kuchambua pamba. Hii ni hatua nzuri ambayo itahakikisha upatikanaji wa pamba kwa vinu vya kuchambua pamba na soko la uhakika kwa wakulima. Natoa wito kwa Ginneries zote kuiga kujenga uhusiano wa aina hii ambao siyo tu una manufaa kwa Ginneries bali pia wakulima.
3. Ndugu
Mwenyekiti, katika kukabiliana na
matatizo yanayoikabili sekta ya kilimo na kupunguza umaskini, Wizara inaendelea
kutekeleza Makakati wa Kendeleza Sekta ya Kilimo. Dira ya Mkakati huu ni kuwa ifikapo mwaka wa
2025, kilimo chetu kiwe cha kisasa, cha kibiashara, chenye tija na chenye faida
na kinachohakikisha matumizi endelevu ya maliasili zilizopo. Lengo ni kuweka mazingira mazuri ya
kuendeleza kilimo chenye faida
4. Upanuzi wa mashamba utawawezesha wakulima kuzalisha kwa wingi na kupata mapato makubwa zaidi kwa eneo kwa kulinganisha na kilimo cha jembe la mkono. Wakulima sasa wataweza kulima eneo kubwa kwa muda mfupi na kutumia muda utakaobaki kufanya shughuli nyingine za kuwaongezea kipato.
5. Ndugu
Mwenyekiti, karibu asilimia 70 ya eneo
linalolimwa nchini linalimwa kwa jembe la mkono, asilimia 20 kwa jembe la
kukokotwa na ng’ombe na asilimia 10 tu kwa trekta. Serikali inahimiza matumizi ya zana bora za
kilimo, hususan matrekta, ili sehemu kubwa ya shughuli za kilimo ifanyike kwa
kutumia mashine badala ya nguvu ya mwanadamu.
Kutokana na umuhimu wa kutumia zana bora za kilimo, natoa wito kwa
wafanyabiashara kuiga mfano wa Tanzania Cotton Association na kuagiza
kwa wingi matrekta na zana nyingine za kilimo.
6. Serikali tayari imeweka vivutio kwa waagizaji wa zana
za kilimo kwa kuwaondolea kodi zote.
Serikali itaendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kuagiza matrekta na
zana zingine za kilimo. Aidha, Serikali
itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwavutia wafanyabiashara kuagiza zana
hizo kadri haja ya kufanya hivyo itakavyojitokeza.
7. Ndugu
Mwenyekiti, wastani wa eneo linalolimwa
mazao bado ni kati ya hekta 0.2 hadi 2 kwa mkulima. Hili ni eneo dogo
8. Kwa
mfano, maeneo yanayolimwa pamba kwa
sasa ni wastani wa kati ya hekta 0.5 na 2.5 na mavuno kwa hekta ni wastani wa
kilo 625 hadi 750 badala ya kilo 3,000 hadi 3,500 kwa hekta
zinazowezekana. Ni lazima tubadilishe
hali hii haraka, kwa kupanua maeneo yanayolimwa na kwa kufuata kanuni za kilimo
bora cha pamba. Wizara yangu itaendelea
kushirikiana na wenye vinu vya kuchambua pamba (Ginners) kuhakikisha
kilimo cha pamba nchini kinapanuka na kinakuwa cha tija kubwa kuliko ilivyo
sasa.
9. Ninapenda kuchukua fursa hii
kuwahakikishia wakulima upatikanaji wa pembejeo wakulima kwa wakati na kwa
kiasi cha kutosha ili juhudi za kupanua mashamba ziende sambamba na upatikanaji
wa pembejeo za kilimo. Kwa kufanya
hivyo, tunatarajia tutapanua maeneo na kuongeza uzalishaji kwa eneo. Wizara yangu itaendelea kuratibu na kusimamia
upatikanaji wa mmbolea na madawa ya kilimo ili yapatikane kwa wakati na kwa bei
nafuu. Kwa mfano, Serikali imeweka
ruzuku kwenye mbolea ili ipatikane kwa bei nafuu ili kuwawezesha wakulima
kuitumia kwa wingi na kupata mazao mengi kwa eneo. Wizara itaendelea kusimamia na kuimarisha
utaratibu huo ili uwanufaishe wakulima wote.
10. Ndugu
Mwenyekiti, suala la ubora wa pamba ni
muhimu ili wakulima wapate bei nzuri kwa pamba wanayolima. Bei za mazao
11. Ndugu
Mwenyekiti, baada ya kusema hayo
machache, ninapenda kuwashukuru tena viongozi wa Tanzania Cotton Association
kwa kunikaribisha kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kuwakabidhi matrekta
kutoka kwa Noble Motors. Napenda
kuwahakikishia ushirikiano wangu na wa Wizara ya Kilimo na Chakula katika
kupanua kilimo cha kutumia zana bora za kilimo.
Msisite kuwasiliana na Wizara yangu kila mtakapouhitaji.
Nawashukuru