HOTUBA YA MHESHIMIWA PROF. P.P. MBAWALA (MB), NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA
KILIMO NA CHAKULA,
WAKATI WA KUFUNGUA WARSHA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA AKIBA
NA MIKOPO (SACCOS) MJINI NAMTUMBO MKOANI
-
-
Maafisa Ushirika
-
Viongozi wa
Chama Tawala cha CCM
-
Viongozi wa
SACCOS Washiriki Warsha
-
Wageni Waalikwa
-
Mabibi na
Mabwana
Awali ya yote
napenda kuwapongeza na kuwakaribisha viongozi wote wa
vyama vya Ushirika vya Akiba
na Mikopo kwa kuchaguliwa kushiriki warsha hii muhimu hapa
Namtumbo ambako ni Makao Makuu
ya Wilaya yetu mpya.
Aidha, nami nitoe
shukrani zangu za dhati kabisa
kwa Waandalizi wa Warsha kwa
kunialika mimi binafsi nikiwa Mbunge wa Wilaya
ya Namtumbo kuifungua Warsha hii. Nasema aksante
Ndugu Mwenyekiti, warsha hii ina
umuhimu wake katika masuala ya uendeshaji
makini wa shughuli za Vyama
vya Akiba na Mikopo au SACCOS. Ujenzi wa Ushirika katika
uchumi wa soko nchini mwetu
unatiliwa maanani
“Chama cha Mapinduzi
kinatambua kuwa Ushirika ndicho chombo cha uhakika cha ukombozi kwa wakulima,
wafugaji na wavuvi wadogo wadogo. Ushirika wa kuweka na
kukopa uliwekewa mkazo kwa sababu
ndicho chombo mwafaka katika kutatua matatizo ya maendeleo ya
wanachama wake.
Kwa mfano upatikanaji wa pembejeo na mikopo”.
Hivyo warsha hii
ni moja ya
mikakati ya mafunzo ya kuuimarisha
ushirika. Kwa kupitia mafunzo ya warsha hii,
tunaimarisha Elimu ya Ushirika kuhusu
kuboresha fani ya menejimenti, uchumi na udhibiti
wa fedha kwa Halmashauri, watumishi na wanachama
juu ya vyama
vyao. Uendeshaji wa SACCOs
kwa umakini sio tu mipango
wa kupanua idadi na wanachama
wa vyama bali pia kwa
usimamizi bora wa vyama hivyo.
Taarifa zilizoko kitaifa zinabaini kuwa matatizo mengi ndani ya ushirika
yanafanana. Ingawa juhudi za
kukabiliana nayo yanategemea na mwamko na uelewa
wa wanaushirika wenyewe mahali walipo. Kwa kifupi baadhi
ya matatizo ni
(1)
Vyama kushindwa
kutoa huduma kwa wanachama wao
za madawa na pembejeo kwa
wakati, na kwa viwango vinavyotosheleza
mahitaji kitaalam.
(2)
Vyama vikuu
haviwajibiki ipasavyo kwa kuvilipa ushuru
wake mapema vyama vya msingi. Matokeo
vinatumia malipo ya fedha za
mkulima kugharimia uendeshaji wake.
(3)
Wanachama, wahalmashauri na watendaji wa Vyama
vya ushirika hawapati elimu ya kutosha kuhusu
ushirika na shughuli zao
(4)
Halmashauri kushindwa kusimamia watendaji kuandika na kufunga vitabu
vya mahesabu kwa wakati kisha
kuviwasilisha kwa wakaguzi kwa muda
unaotakiwa kwa mujibu wa sheria. Aidha, wanachama hawasomewi mahesabu
(5)
Wizi na
udanganyifu ambao unafanywa na watendaji
wasio waaminifu ndani ya ushirika
umedhohofisha
(6)
Vyama vya
ushirika havikaguliwi mara kwa mara
hivyo kukosa usimamizi wa karibu
wa sheria na kanuni za
ushirika katika vyama hivyo.
(7)
Wanachama na
viongozi wa vyama kutoheshimu misingi ya kidemokrasia
wakati wanachagua/kubadilisha
viongozi katika vyama vyao.
(8)
Vyama havina
mitaji ya kutosha kutokana na kuwa na
wanachama wachache na kuweka viwango
vya chini vya hisa zao.
(9)
Wananchi hukatishwa
tamaa na Vyama vya Ushirika
dhaifu na hivyo idadi ya
wanachama wanaojiunga na vyama vya
ushirika haiongezeki na hata hisa
za wanachama vyamani haziongezeki.
(10)
Viongozi na
watendaji wababaishaji hujipenyeza katika Vyama vya ushirika
na kusababisha gharama kubwa za
uendeshaji na usimamizi bila kujali maslahi ya wanachama.
Ndugu Mwenyekiti, sera ya maendeleo ya
ushirika inatambua fika kuwa vyama
vya ushirika ni taasisi binafsi
lakini serikali haiwezi kupuuzia matatizo haya. Aidha ni jukumu la wanachama
wenyewe na hasa ninyi viongozi
kuhakikisha matatizo
Mafanikio ya SACCOs
yatatokea haraka ikiwa Wanachama watajenga tabia ya kuweka akiba
kwa maendeleo ya kiuchumi na
kijamii ya wanachama kwa wakati
uliopo na siku za usoni. Uwekaji fedha katika SACCOs
itasaidia wanachama kupata mikopo tena
kwa masharti nafuu ukilinganishwa na upatikanaji wa fedha hizo
toka Benki kwa masharti magumu
yanayotolewa au asasi nyingine za fedha
zinazotoa riba kati ya asilimia
12 na asilimia 24, tozo ambalo wananchi
au wakulima wengi wenye kipato kidogo
wanashindwa kutimiza masharti hayo.
Katika mkakati wa kupata mitaji
zaidi ya kuwapatia wanachama wa SACCOs kwa
masharti nafuu, SACCOs ziwe na
uhusiano wa karibu
Pamoja na mafanikio
niliyoyataja vyama hivyo itabidi viendelee
kuwa na sifa
za kukopesheka, maana yake viweze
kutumia fedha hizo kwa kukopesha
wanachama wake na kurejesha mikopo kwa wakati bila
ya ubabaishaji, ili fedha hizo
zizunguke kwa kuwasidia wengine. Tegemeo langu warsha hii
itawezesha pia kuwapa uwezo wa
kuendesha na kusimamia shughuli za SACCOs kwa
makini kusudi SACCOs zenu ziweze
kuwa vyama vya Akiba na
Mikopo ambavyo ni endelevu na
zinazoelekeza rasilimali zao adimu kwenye
shughuli za manufaa kwa maslahi
ya wanachama. Mkitaka SACCOs zenu zizidi
kushamiri inabidi kuwepo na nidhamu
ya matumizi mazuri ya mikopo
inayotolewa. Urejeshaji mikopo hiyo inayotolewa
uwe kwa asili
mia moja kusudi wengine waweze kuwa na
mitaji ya kukidhi mahitaji yao, iwe katika
shughuli za kilimo,biashara na shughuli zingine, mfano ujenzi wa
nyumba bora au ununuzi wa pembejeo
au hata kulipia ada za shule.
Mwisho, Mwenyekiti naomba nirudie tena kuwashukuru kwa kuja kuhudhuria
warsha hii kwa lengo la kutoa
huduma bora katika SACCOs zenu. Niwapongeze tena waandaji wa
warsha hii ambayo naitakia mafanikio makubwa.
Baada ya kusema
hayo mafupi sasa napenda kutamka
rasmi kuwa warsha yenu imefunguliwa
rasmi.
Aksanteni kwa kunisikiliza.