Mhe. Pius Mbawala, Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula,
Ndugu Katibu Mkuu,
Ndugu Wafanyakazi,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Ndugu Mwenyekiti, awali ya yote, ninapenda nichukue nafasi hii kukushukuru
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pamoja na Uongozi wote wa Mkoa
kwa kutupokea vizuri. Ninakushukuru pia kwa kushiriki katika mkutano huu. Ninapenda kuchukua fursa
hii kuwashukuru nyote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria
Mkutano Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Chakula. Aidha, ninapenda niwashukuru wale
wote walioshiriki katika kuandaa mkutano huu kwa kazi
nzuri waliyofanya.
2. Ndugu
Mwenyekiti,
3. Ndugu
Mwenyekiti, sababu
nyingine ya kukutana kila mwaka ni kutathmini mtazamo wetu kuhusu kilimo na
kuona
4. Ndugu
Mwenyekiti, karibu
asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini ambako wanategemea kilimo kwa maisha
5. Ndugu
Mwenyekiti, katika
miaka minne iliyopita, kilimo kimeanza kuonyesha dalili za kuongeza kasi ya
kukua. Kasi hiyo imeongezeka kutoka
asilimia 4.1 mwaka wa 1999 na kufikia asilimia 5.5
mwaka wa 2003. Inatarajiwa kwamba ukuaji
huo utafikia asilimia sita mwaka wa 2003. Hata hivyo, kiasi hiki cha ukuaji bado ni kidogo kuondoa umaskini na kuwezesha uchumi kukua kwa
kasi ya kuridhisha. Changamoto iliyo
mbele yetu ni kukifanya kikue kwa kasi ya asilimia 10
au zaidi kwa mwaka. Kazi iliyo mbele
yetu ni kubaini njia zitakazokifikisha kilimo kwenye
kiwango hicho cha ukuaji.
6. Katika
hutoba yangu ya mwaka jana, niliainisha matatizo
mbalimbali yanayokikabili kilimo. Aidha,
katika mkutano huo mlipata fursa ya kujadili matatizo hayo na
mengine mengi yanayokwamisha kilimo na kupendekeza njia za kuchukua
kuyatatua. Mkutano huu ni fursa nyingine ya kutathmini jinsi tulivyokabiliana na
matatizo hayo, mafanikio tuliyoyapata na hatua za kuchukua kwa matatizo ambayo
yanaendelea kuathiri maendeleo ya kilimo.
Itakuwa vizuri
7.
Ndugu Mwenyekiti, pamoja na kwamba mwaka jana nilitaja matatizo
yanayokikabili kilimo, ningependa hata mwaka huu nichangie katika mkutano huu
kwa kuyataja tena kwani bado yapo. Tatizo moja wapo ambalo itabidi tupambane
nalo ni tabia potofu ya kubeza na kudharau
kilimo. Kutokana na
tabia hiyo, kilimo kimekuwa hakipewi umuhimu katika mipango ya maendeleo na
hivyo kutokutengewa raslimali za kutosha. Kwa mfano, Halmashauri nyingi za
Mitaa hupata mapato
8.
Mchango mdogo wa kilimo cha umwagiliaji maji
mashambani kwa kulinganisha na eneo linalofaa kuendelezwa kwa ajili ya
umwagiliaji.
9.
Teknolojia nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa na
Vituo Vyetu vya utafiti zimekuwa haziwafikii wakulima. Aidha, unganisho hafifu
kati ya utafiti, mafunzo, huduma za ugani na wakulima limesababisha teknolojia
hizo na mbinu bora za uzalishaji na usindikaji kutowafikia wakulima wengi.
Aidha, kutokuwapo kwa mbinu sahihi ya kutoa mbinu za
ugani kumechangia kwa kiwango katika tatizo
10.
Upotevu wa mazo kabla na baada ya mavuno ni
tatizo ambalo halijapatiwa ufumbuzi wa kutosha. Visumbufu vya mimea na mazao vimeendelea kusababisha upotevu mkubwa kutokana na
wakulima kutozifahamu mbinu mbalimbali za kudhibiti visumbufu hao. Aidha, uhaba wa
miundombinu ya kutosha kwa ajili ya kuzindika mazao ni tatizo linalochangia kwa
kiasi kikubwa katika upotevu wa mazao, husani yale yanayoharibika haraka
11.
Kilimo cha kutumia zana duni na matumizi madogo
ya pembejeo ni kikwazo kikubwa katika kuongeza tija na uzalishaji katika
kilimo. Matumizi ya matrekta, majembe
ya kukokotwa na wanyama na mashine bora za kurahisisha
kazi bado ni madogo. Kutokana na tatizo hili, wakulima
wengi wana mashamba madogo ya kati ya hekta 0.2 hadi 2.0. Hivyo, wakulima wa
aina hii hawawezi kupanua eneo wanalolima na uzalishaji katika vishamba hivyo
ni wa kujikimu.
12. Pamoja
na matatizo niliyoyataja na mengine mengi ambayo
mmekuwa mkipambana nayo, yapo pia mafanikio ambayo yamepatikana. Mafanikio hayo yametokana na
juhudi zenu kwa kushirikiana na wafanyakazi wengine na wadau mbalimbali katika
sekta ya kilimo. Ninapenda
kuchua fursa hii kuwapongeza wote waliowezesha mafanikio hayo kupatikana.
13. Baadhi
ya mafanikio yaliyopatikana ni;
(i)
Kukamilika
kwa maandalizi ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo, kwa ngazi ya Taifa,
ambayo iliandaliwa na Wizara ya Kilimo na Chakula kwa kushirikiana na Wizara za
Maji na Maendeleo ya Mifugo na Ushirika na Masoko, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa na washirika wa maendeleo ambao wamekuwa
wakishirikiana au wanakusudia kushirikiana na Wizara katika kutekeleza majukumu
yake.
(ii)
Kukamilika
kwa maandalizi ya sehemu ya kwanza ya Mpango Kabambe
wa Umwagiliaji Maji Mashambani.
Mafanikio ya awali ya maandalizi hayo yamekamilika na sasa tnajua kuwa
Taifa lina hekta milioni 29.2 zinazofaa kuendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji
maji mashambani na
siyo hekta milioni moja
(iii)
Wizara
kwa kushirikiana na walengwa katika maeneo mbalimbali
ya nchi imekamilisha miradi 28 ya umwagiliaji maji mashambani na mingine
inaendelea kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
(iv)
Katika
kukabiliana na kero ya watumishi kutopandishwa vyeo kwa muda mrefu, wizara
imeweka utaratibu mzuri wa kupata takwimu na taarifa za utendaji kazi za
watumishi kwa kila mwaka na tayari watumishi wengi wamepandishwa vyeo kwa
mserereko na wale ambao hawajapandishwa vyeo tunatarajia wapate stahili zao
kabla ya mwisho wa Juni, 2003. Wizara
inakusudia kuendelea kurekebisha na kuboresha maslahi
ya watumishi wake ili yaende sambamba na watumishi wenye sifa
(v)
Vituo
vya Utafiti vimekuwa vikitoa teknolojia bora ambazo zikiwafikia wakulima
zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mapinduzi
ya kilimo. Kwa mfano, vituo vimezalisha
mbegu bora za mazao mbalimbali ambazo zikizalishwa kwa
wingi zitaongeza uzalishaji katika kilimo kwa kiasi kikubwa. Kwa kutumia mbinu shirikishi jamii,
tutahakikisha teknolojia hizo zinawafikia wakulima.
(vi)
Wizara
kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa na wakulima
imeimarisha uwezo wa kupambana na visumbufu vya mimea na mazao na kudhibiti
milipuko ya visumbufu hivyo ili ilipojitokeza. Aidha, wizara imeendelea kueneza
matumizi ya mbinu ya udhibiti husishi na itaendelea
kufanya hivyo.
(vii)
Kuweka
mfumo wa huduma za ugani wenye ufanisi. Wizara
inakusudia kuhakikisha matumizi ya mbinu shirikishi jamii na shamba darasa yanaenezwa nchi nzima. Mafanikio
makubwa yaliyotokana na matumizi ya mbinu hizi katika
maeneo nchini, yamedhihirisha kuwa mbinu hizo zinafaa kutumika nchi nzima.
14. Ndugu mwenyekiti, kilimo chetu
kimeanza kuonyesha dalili za kukua japokuwa kinaendelea kuathiriwa vibaya na matatizo mbalimbali yakiwemo ya hali mbaya ya hewa.
(i)
Kila mkulima au kaya ya wakulima inakuwa na shamba
lenye ukubwa wa kutosha
(ii)
Kuweka utaratibu shirikishi jamii wa
kuandaa mipango ya kilimo na usimamizi wake katika ngazi zote ili kuhakikisha
wananchi wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji na kumiliki mipango hiyo.
(iii)
Kuweka mfumo utakaohakikisha upatikanaji wa mahitaji ya kilimo ikiwa ni pamoja na mikopo kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za kilimo.
(iv)
Kuhimiza matumizi ya wanyama kazi na
zana za kisasa katika uzalishaji na usindikaji wa mazao.
(v)
Kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa, hususan
sayansi ya bioteknolojia.
(vi)
Kupunguza upotevu wa mazao
kabla na baada ya mavuno kwa kutumia mbinu husishi na teknolojia bora za
kudhibiti visumbufu vya mimea na mazao.
(vii)
Kuunganisha na kuimarisha
huduma za utafiti, ugani na mafunzo ili kuondoa udhaifu uliokuwapo katika
unganisho (linkage) la huduma hizo.
(viii)
Kuboresha na kuweka mfumo
imara wa uapatikanaji na usambazaji wa pembeo za kilimo. Wizara itaendelea
kuwasiliana na mamlaka husika ili kuharakisha
uanzishwaji wa Wakala wa mbegu.
(ix)
Kuhimiza uzalishaji, kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa
na soko, wa mazao ya biashara yasiyokuwa ya asili kama vile mazao ya viungo,
maua na matunda ambayo yana bei nzuri.
(x)
Kuhimiza na kufundisha kilimo
cha kibiashara ili wakulima waendeshe shughuli za kilimo kwa faida na kwa
kuzingatia gharama halisi za uzalishaji.
14. Ndugu
Mwenyekiti, hayo
niliyoyataja ni baadhi tu ya matatizo na mafanikio
yaliyojitokeza miaka ya hivi karibuni.
Wakati mnajadili mada mbalimbali mtapata fursa ya kuchangia mawazo yanu
katika maeneo niliyogusia na mengine yatakayojitokeza
katika mada hizo. Ningependa wahiriki
wote wa Mkutano huu watoe mawazo
15. Ndugu Mwenyekeiti, kabla sijamaliza
hotuba yangu ninapenda kutumia fursa hii kutoa taadhari kwa
wananchi kutumia vizuri chakula walichojiwekea. Taarifa
zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka huu inawezekana tusipate mvua ya kutosha. Kuna dalili kwamba baadhi ya sehemu za nchi
zitapata ukame au mvua zitanyesha kwa mtawanyiko
mbaya. Hivyo, wakulima
washauriwe kulima mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam
utakaotolewa na watalaam wa kilimo kwenye maeneo
16. Ndugu Mwenyekiti, baada ya kusema
hayo ninapenda kuwashukuru maandalizi na mapokezi mazuri tuliyoyapata. Aidha, ninawatakia majadiliano yenye manufaaa. Sasa natangaza kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wafanyakazi wa
Kilimo umefunguliwa rasmi.