HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO NA
CHAKULA,
MHE. CHARLES N. KEENJA (MB.) WAKATI
AKIFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI, MJINI MOROGORO, TAREHE 19 MACHI,
2004
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Waheshimiwa Viongozi wa Wizara ya Kilimo na
Chakula,
Waheshimiwa Washiriki wa Baraza
1. Awali ya yote, ninapenda kuwashukuru kwa
kunialika kuja kufungua Mkutano wa Baraza lenu la Wafanyakazi wa Kilimo. Hii ni fursa nzuri kwangu kutoa mchango wangu
wa mawazo na ni nafasi nzuri ya kupata taarifa, kuelekezana kukumbushana na
kuchangia mawazo kuhusu majukumu ya Wizara na ushiriki kwa wafanyakazi katika
kuyatekeleza na kuyasimamia.
2. Mwenyekiti, Baraza la Wafanyakazi ni
chombo kinachowawezesha wafanyakazi kushiriki katika mipango na utekelezaji
wake. Mabaraza ya wafanyakazi hutoa
fursa kwa wafanyakazi kushiriki katika maamuzi mbalimbali na kuboresha uhusiano
baina ya wafanyakazi mahali pa kazi. Kwa
maneno rahisi ni chombo cha kuimarisha na kuboresha demokrasia mahali pa kazi. Hata hivyo inatubidi kuwa na tafsiri sahihi
ya demokrasia mahali pa kazi.
3. Demokrasia ninayoizungumzia ni mfumo
unaowawezesha wafanyakazi kushiriki katika kufanya maamuzi halali na kutekeleza
maamuzi hayo kwa wakati uliopangwa, kwa uadilifu na kwa nidhamu ya hali ya juu
ya kazi. Ni mfumo unaoweka mizania sawa
kati ya maslahi ya mwajiri na mwajiriwa.
Kwa maneno mengine ni mfumo unaoweka wajibu na haki za kila mwajiri na
mwajiriwa katika kufanikisha malengo ya kiuchumi na kijamii.
4. Ndugu Mwenyekiti, nchi yetu imepitia mfumo
wa uchumi hodhi na sasa wanuchumi huru na utandawazi. Misingi na mahitaji ya mifumo hii
yanatofautiana kwa baadhi ya mambo.
Hivyo, kuna haja ya kuifahamu vizuri na kubadili fikira zetu na
utaratibu wa utendaji kazi ili kazi zetu ziwe za ufanisi. Kubadilika kutoka mfumo mmoja kwenda mfumo
mwingine, mara nyingi husababisha woga na wasiwasi kuhusu matokeo ya mfumo
mpya. Mfumo wa sasa wa soko huru
haukwepeki
5. Ndugu Mwenyekiti, Taifa letu liko katika
mabadiliko na linafanya mabadiliko katika sera, miundo ya taasisi zetu na sheria
mbalimbali zinazosimamia utekelezaji wa sera zetu. Kwa mfano, tunao Mpango wa Kurekebisha
Utumishi wa Umma (Civil Service Reform). Mipango ya Kurekebisha Serikali za Mitaa na
Mashirika ya Umma, Mipango hii inatutaka tubadilishe utendaji wetu wa kazi na
hata fikra zetu kuhusu kazi. Baraza la
Wafanyakazi linabidi kuwa mstari wa mbele kuelewa na kuwaelimisha wafanyakazi
wengine juu ya umuhimu na matokeo ya mipango hii, ili wafanyakazi washiriki
kikamilifu katika kuifanikisha.
6. Ni wazi katika kutekeleza mipango hii,
kutakuwa na vikwazo na matatizo yatakayojitokeza. Hata hivyo, vikwazo hivyo na matatizo
yatakayojitokeza inabidi kuwa changamoto katika uendeshaji wa shughuli za
Serikali. Baraza linabidi liwe mshiriki
mkubwa katika kubuni mbinu mpya za uendeshaji wa shughuli za Serikali, na siyo
kusubiri tu Serikali kubuni mbinu za uendeshaji wa shughuli zake na Baraza
kufanya kazi ya kupokea malalamiko tu kutoka kwa wafanyakazi.
7. Ndugu Mwenyekiti, nchi yetu inaendesha
mfumo wa Vyama vingi vya Siasa.
Wafanyakazi inabidi wafahamu vizuri mfumo wa vyama avingi vya siasa na
jinsi ya kautekeleza majukumu
8. Baraza la Wafanyakazi linabidi kuelewa
kwa ufasaa mipango mbalimbali ya Serikali na kuwaelimisha watumishi wengine
kuhusu mipango hiyo. Kwa mfano, Baraza
la Wafanyakazi wa Kilimo linabidi kuelewa Sera ya Kilimo, Mkakati wa Kuendeleza
Sekta ya Kilimo, Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo, na jinsi Wizara
inavyotelekeza majukumu yake kwa kufuata sera, mkakati na Mipango iliyopo.
9. Ndugu Mwenyekiti, hizi ni zama za
utandawazi. Inatubidi kuuelewa
utandawazi na kuandaa mikakati itakayohakikisha nchi yetu inanufaika na
utandawazi. Utandawazi unatutaka tufanye
kazi tofauti na mazoea tuliyokuwa nayo huko nyuma. Inatubidi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kwa
nidhamu ya kazi ya hali ya juu na kwa kusimamiana. Mazingira ya kazi yamebadilika
10. Ndugu Mwenyekiti, teknolojia bora ni nyenzo
nzuri ya kuongeza ufanisi sehemu za kazi na motisha kwa wanaozitumia. Hata hivyo, teknolojia hizo zitakuwa za
manufaa
11. Ndugu Mwenyekiti, nimekuwa nikikutana na
wafanyakazi wengi ambao wamekuwa wakijitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa
Kilimo. Lakini nimekuwa nikijiuliza
12. Ndugu Mwenyekiti, ninafahamu kuwa moja ya
mambo mtakayojadili ni makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo na Chakula. Hii ni fursa nzuri kwenu kutathmini shughuli
zilizotekelezwa mwaka huu na matokeo ya shughuli hizo. Aidha, ni wakati mzuri wa kuainisha maeneo
muhimu ya kupewa kipaumbele katika mwaka wa 2004/2005. Maeneo hayo yawe ni yale ambayo
13. Eneo lingine ninalopenda
kutiliwa mkazo ni kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa kilimo. Hii ni pamoja na kukamilisha zoezi la
kuwapandisha vyeo watumishi wa kilimo na kurekebisha maslahi yao kulingana na
sifa walizonazo, kuwapatia vitendea kazi na kutoa miongozo mbalimbali
itakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Inatubidi kuangalia wafanyakazi kama
raslimali muhimu katika kuendeleza kilimo na kwa hiyo kuna haja ya kuiendeleza
na kuijengea mazingira mazuri ya kazi.
14. Ndugu Mwenyekiti, kilimo chetu bado
hakijakua kwa kasi itakayotuwezesha kujitosheleza kwa chakula na kuhimili
athari zinazosababishwa na ukame, milipuko ya visumbufu vya mimea na mazao na
majanga mengine. Aidha, hakijakua kwa kasi
ya kupunguza umaskini kwa wanaokitegemea kilimo kwa maisha yao. Hii ina maana kwamba kuna mambo ambayo
hatujafanya au hatujafanya sawa sawa kukifanya kilimo kikue kwa kasi
inayotakiwa. Hii ni changamoto ambayo
inabidi kuijadili na kuona kama mipango iliyopo inakidhi mahitaji ya sasa ya
kilimo.
15. Kabla sijamaliza hotuba yangu napenda
kuwakumbusha kuwa tunazo raslimali ambazo ni lazima tuziwekee mipango mizuri
ili ziwezeshe kilimo kukua kwa kasi kubwa kuliko ilivyo sasa. Tuna raslimali ya watu, ardhi, maji na mitaji
kutoka vyanzo mbalimbali. Raslimali hizi
hatujazitumia kikamilifu kutuwezesha kufikia kiwango cha ukuaji wa sekta ya
kilimo utakaotuwezesha kuondokana na umaskini.
Aidha, matumizi ya muda kama raslimali muhimu hatujaitilia maanani sana. Mipango ya kutumia raslimali lazima ijumuishe
matumizi ya muda. Lazima tuandae mipango
mizuri itakayotuwezesha kutumia raslimali tulizonazo kwa manufaa yetu na vizazi
vijavyo. Mahali pa kuanzia ni kwenye
bajeti ya kilimo na raslimali ya watu tuliyonayo.
16. Mwisho, baada ya kusema hayo
machache sasa natangaza kuwa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Kilimo
umefunguliwa rasmi. Nawatakia
majadiliano yenye mafanikio.
Asanteni kwa kunisikiliza.