Skip to main content
Habari na Matukio

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA PILI YA KUTUMA MAOMBI KUJIUNGA VYUO VYA MAFUNZO YA KILIMO-2017/18

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA PILI YA KUTUMA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VYA MAFUNZO YA KILIMO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) anautangazia Umma kuwa Wizara kupitia Vyuo vyake vya Mafunzo ya Kilimo nchini, imeongeza muda wa kudahili Wanafunzi kwa ajili ya Muhula wa Mafunzo kwa Mwaka 2017/2018 hii ni baada ya zoezi la kuchangua Wanafunzi Awamu ya Kwanza kumalizika na kuonekana kuwa Vyuo bado vina nafasi ya kudahili Wanafunzi wapya, kutokana na hali hiyo, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)  limeruhusu Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo kudahili Wanafunzi zaidi ili kujaza nafasi hizo.

Kupitia tangazo hili. Wahitimu wa Kidato cha Nne na Sita na wengine wenye sifa za kuomba nafasi hizo, wanatakiwa kutuma maombi yao haraka iwezekanavyo au unaweza kuwasiliana na Chuo cha Kilimo kilichokaribu yako kwa maelezo zaidi.

Aidha, maombi ya kujiunga na Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo katika kozi ya Stashahada na Astashahada yamefunguliwa kuanzia Tarehe 18 Septemba, 2017 mpaka tarehe 1  Oktoba, 2017.  Maombi yatumwe kwenye Vyuoni husika.

Fomu ya maombi na orodha ya Vyuo vya Kilimo zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO); ambayo ni (www.kilimo.go.tz) au kupitia link hii........

 

Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO)

Pakua Faili: