Skip to main content
Habari na Matukio

WAZIRI BASHE ATOA ONYO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KUHUJUMU BIASHARA YA MAZAO YA WAKULIMA.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amewataka Wakulima kuwa huru kuuza mazao na kukataza tabia ya baadhi ya viongozi wa Vyama vya Ushirika kuhujumu mazao ya Wakulima kwenye Vyama hivyo.

Ameyasema hayo  wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassani Wilayani Chunya jijini Mbeya,

Amesema Wakulima pindi wanapo vuna mazao yao na kupelekea kwenye Vyama vyao vya Ushirika, baadhi ya viongozi wanachukua rushwa kwa wanunuzi Ili kuweza kushusha bei ya mazao na kumpa hasara mkulima.

Waziri Bashe ameitaja Kampuni ya Primer ambao ni wanunuzi wa Tumbaku kwa wakulima na wamekuwa na tabia hiyo ya kutoa rushwa kwa viongozi wa Ushirika ili wapate nafuu ya bei ya kununua Tumbaku.

Aidha Waziri Bashe akiwa katika Kata ya Chalagwa Wilayani Chunya, aliwataka Wakulima kuondoa hofu juu ya kupanda kwa bei ya Mbolea na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeandaa mpango wa luzuku ya mbolea kwa wakulima na utazinduliwa tarehe 08/08 mwaka huu katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wakulima (NaneNane) lengo ikiwa ni kumpatia mkulima nafuu ya ununuzi wa mbolea.

"Serikali ya Mama Samia ni Skivu sana na inawajali wananchi hususani Wakulima na mwaka huu tumeongezewa bajeti kubwa sana haijawaitokea lengo ni kuboresha Biashara ya Kilimo nchini hivyo nawasihi Wakulima wenzangu limeni, uzeni popote pale lakin hakikisheni mnabakisha chakula Cha nyumbani na mimi sitafunga mpaka". Alisema Waziri Bashe