Skip to main content
Habari na Matukio

BASHE AWATAKA MAAFISA UGANI KUTUMIA FOMU MAALUM KUKUSANYA TAARIFA ZA WAKULIMA

 Na Bashiri Salum,Wizara ya kilimo

Shinyanga  

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Husseni Bashe leo 01.10.2019 amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi  Zeinabu Telaki fomu maalumu  (call sheet ) ambayo itatumiwa na Maafisa Ugani  wakati wa kuwatembelea wakulima  na kujaza  taarifa zao muhimu zikiwemo namba za simu, aina ya mazao anayolima,mbolea wanayotumia  pamoja na changamoto zinazowakabili .

Akizungumza  wakati wa makabidhiano hayo Mhe,Naibu Waziri amesema kwamba Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru kitapita  kila Halmashauri katika Ukanda wote inapolimwa pamba na kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya Maafisa watendaji  wa Vijiji ili kusaidia na kushauri shughuli za kilimo ngazi ya chini.

Amesema  zoezi hili litaisida kupunguza tatizo la ukosefu wa Maafisa Ugani ambao wangeweza kushauri wakulima.

Aidha amesisitiza kwamba kila Afisa Kilimo wa Kata au Kijiji atatakiwa kutembelea wakulima wasiopungua watano (5) na kuchukua taarifa muhimu zikiwemo  majina ya wakulima ukubwa wa shamba, aina ya kilimo kinachofanyika, mbolea iliyotumika mwaka jana  na mawasiliano ya mkulima.

Hata hivyo amemsahuri mkuu wa Mkoa huo kukutana na wenyeviti wa Halmashauri ili kujadili  uanzishwaji wa mashamba  ya mfano yatakayomilikiwa na Halmashauri hizo ili wakulima waweze kuyatembelea na kujifunza kilimo cha kitaalamu.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Bashe amesema umefika wakati ambao zao la pamaba linatakiwa lijitegemee kama yalivyo mazao mengine na serikali imejipanga kuleta viuatilifu kwa wakati na kwa bei nafuu ili wakulima waweze kununua .

Hata hivyo Mhe. Bashe amewatoa hofu wakullima kuhusu upandaji wa bei za mbegu  amesema mwaka huu bei haitafika shilingi 1,000 bali itakuwa katika ya sh. 600 na 650 iwe kama namna ya kupunguza machungu ambayo wakulima wa pamba wameyapata kwa mwaka huu.

Amewataka wataalamu wa kilimo kusaidia kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka miche 7,000  hadi 20,000 kwa ekari  kwa kuwa kutasaidia kuondoa tatizo la bei ya pamba  kwa sababu pamba itakuwa nyingi kwa ekari.

Aidha Mhe. Bashe  amezishauri Halmashuri nchini kote kujenga  maghala kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya wakulima baada ya mavuno ili kuondokana na changamoto za mara kwa mara wakati wa mvua

 Naye Mkuu wa Mkoa huo Bi Zainabu Telaki amesema, sasa wameanza jitihada za kuhamia katika kilimo cha umwagiliaji kutokana na uhaba wa mvua katika mkoa huo na kuiomba wizara ya kilimo kusaidia upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji.

Katika zoezi la ununuzi wa pamba Bi Telaki anasema pamba nyingi ya mkoani kwake  imenunuliwa isipokuwa kawma walikuwepo wakulima walioficha majumbania na ile ambayo ilibainika kupenyezwa  kinyemela kutoka Mikoa ya jirani wakitafuta soko.

kama kuna pamba iliyobaki "itakuwa ni kidogo sana katika baadhi ya AMCOS  na kwa wale ambao walificha ili ipande bei"alisema Bi Telaki

amesema wakulima wengi mkoani humo ikiwemo wilaya ya Kishapu washaanzana kuandaa msimu wa kilimo hivyo amemumba Naibu Waziri kusaidia pembejeo zifike kwa wakati ili wakulima hao wawahi mvua za kwanza.

Awali Mhe. Bashe aliagazi Iadara ya Mazao iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo (DCD)kufanya tathmini kwenye sikimu zote katika mkoa huo ili Kujua idadi ya skimu zinazohitaji marekebisho na zinahitaji kujengwa upya.

mwisho