Skip to main content
Habari na Matukio

HALI YA UINGIZAJI NA USAMBAZAJI WA MBOLEA HAPA NCHINI

HALI YA UINGIZAJI NA USAMBAZAJI WA MBOLEA HAPA NCHINI

 

Katika msumu ulipita wa 2016/17 serikali iliagiza kiasi cha tani 159,424  ambapo kati ya hizo tani 37,272 zilisafirishwa kwenda nchi za nje kwa utaratibu uliowekwa.

Aidha, kiasi cha tani 122,152  za mbolea zilisambazwa katika mikoa mbalimbali na kuwafikia wakulima hapa nchini

Katika taarifa yake Mtendaji kuu wa Mamlaka ya mbolea bwana Lazaro Kitandu anasema, Pamoja na mwitikio wa wakulima katika kutumia mbolea hapa nchini lakini msimu ulipita wa 2016/17  tani 122,152 za mbolea ambazo zilikuwepo hapa nchini, wakulima walitumia tani 88,752 tu hivyo tani 33,400 za aina ya urea zilibaki (carry over stock)

Katika msimu wa  2017/2018 akiba ya mbolea iliyobaki msimu uliopita  ambayo ni tani 33,400, kabla ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja kuanza, serikali ilitoa vibali kwa watu wafanyabiashara wa mbolea kuagiza tani 35,000 za mbolea ya aina ya urea ili kuendelea na usambazaji wakati uagizaji wa pamoja (BPS) unakamilisha taratibu zake.

Baada ya mfomo wa BPS (Bulk Procurement System) kukamilisha taratibu husika serikali kupitia mfumo huo  ikaagiza tani 32,000 za urea na kufanya kuwa na jumla ya tani 100,400 za mbolea ya urea hapa nchini.

Aidha,  kiasi cha mbolea iliyotumika msimu wa mwaka jana ikilinganishwa na mbolea iliyotumika kwa msimu huu inabainisha kwamba msimu wa 2017/18 tayari imeshazidi kwa 12% ya jumla ya mbolea iliyotumika msimu uliopita kabla hata kufika mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo , mbolea nyingine ya urea tani 20,000 kupitia BPS itaingizwa tarehe 18, Februari 2018. Ili kuongeza wingi wa mbolea nchini, mwezi Machi 2018, mbolea  nyingine tani 35,000 itaingizwa kupitia BPS .   

Kutokana na ongezeko la matumizi ya mbolea kwa wakulima kufuatia punguzo kubwa la bei, matumizi ya mbolea hii yanatarajiwa kuongezeka kwa 45% ifikapo mwisho wa msimu huu wa 2017/2018.