Skip to main content
Habari na Matukio

MIRADI YA UMWAGILIAJI KUANZA CHATO.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe awahakikishia Wananchi wa Chato juu ya kuanza miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji ambayo italeta ukombozi wa kiuchumi.

Ameyasema hayo  alipopewa nafasi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasalimia Wananchi wa kata ya Bwanga, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

“Mkoa wa Geita Mhe. Rais, tunatangaza miradi minne ya Umwagiliaji yenye jumla ya hekta 3400 ili Wananchi walime mwaka mzima.

Aidha, Waziri Bashe aliongeza kwa kuwahakikishia Wananchi kuwa Serikali ya awamu ya sita imedhamilia kuondoa matatizo ya Wakulima na kuwajengea mazingira rafiki katika shughuli zao za Kilimo.

Waziri Bashe pia amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2022/2023 Serikali itaanza kutoa rudhuku ya mbolea.