Skip to main content

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda (Mb) ametoa tathmini ya kazi ya kuwadhibiti nzige wa jangwani waliovamia nchi mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu na kuwa hadi sasa wamedhibitiwa na wataalam wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana  na halmashauri za wilaya za Longido, Siha na Simanjiro.

Prof. Mkenda ameeleza hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari Moshi mkoani Kilimanjaro kuwa mapambano dhidi ya nzige yanaendelea vizuri na kuwa hadi sasa hakuna madhara yoyote kwenye maeneo ya kilimo na mifugo ya wananchi na kuwa jitihada za kuangamiza makundi  yaliyobakia zinaendelea kwa kutumia helkopita na mabomba ya kupiliza kwa mikono.

“Tupo makini kuwakabili nzige hadi sasa hatujapata madhara yoyote kwa mashamba ya wakulima hivyo watanzania wasiwe na taharuki “alisisitiza Prof. Mkenda.

Kuhusu mikakati ya kupambana na nzige Waziri Mkenda amesema hadi leo tarehe 01 Machi tayari kuna helkopta kutoka Shirika la Nzige Wekundu (RLCO) na kuwa serikali itaongeza ndege ya pili kutoka shirika la Nzige wa Jangwani (DLCO) kupulizia makundi madogo ya nzige walionekana maeneo ya wilaya za Longido kufuatia uwepo wa taarifa kuwa nzige wachanga kutoka Kaunti ya Machakos nchini Kenya wanaweza ingia Longido.

Mwisho.

Revocatus Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini