WAZIRI BASHE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe mekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Kyle Nunas.
Waziri Bashe na Balozi Nunas wamejadiliana namna bora ya kuwekeza katika sekta ya kilimo husan uzalishaji wa ngano ili kupunguza upungufu wa ngano hapa nchini.
Mhe. Bashe amemkaribisha Balozi Nunas pamoja na sekta binafsi ya Canada kushiriki Mkutato utakaofanyika Septemba 4 hadi 8 jijini Dar esa Salaam, utakaojadili mifumo ya chakula kwa nchi za Afrika(Africa's Food Systems Forum 2023 Summit) ambao pia utakuwa na malengo ya kukuza biashara ya chakula.
Balozi Nunas aliyeambatana na Kansela Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ubalozi wa Canada, Helen Fytche ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo katika mwaka wa fedha 2023/2024 na Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) yenye lengo la kuwashirikisha Vijana na Wanawake kwenye sekta ya Kilimo.