Skip to main content
Habari na Matukio

Hassunga Aendesha Mkutano wa Uandaaji wa Sera Mpya ya Kilimo

Waziri wa Kilimo Mhe. Japheti Hassunga leo (16.09.2019) amekutana na Menejimenti ya wizara,wakuu wa Taasisi na  Wenyeviti wa Bodi za Mazao  zilizopo chini  ya Wizara.

Lengo la mkutano huu wa siku mbili unaofanyika  katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma  ni kujadili taarifa za utekelezaji za mwaka mwaka 2018/2019 na  maoni kujadili   uandaaji wa sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019

Akiongea katika kikao kazi hicho Mhe. Waziri  Hasunga ameeleza umuhimu wa sera hiyo unalenga kukifanya kilimo kuwa na tija na cha kibiashara sera hivyo kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo

Mhe. Waziri amebainisha kwamba sera hiyo inatakiwa kukamilika  mapema mwaka huu ili kutoa fursa ya kuandaa sheria na kanuni za kilimo.

Kikao hicho kinahudhuriwa na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba,Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu Prof.Siza Tumbo.

Mwisho.