Skip to main content
Miongozo
Swahili

Utaratibu wa kuomba vibali vya kusafirisha chakula nje ya nchi

  1. Mwombaji lazima awe na TIN No.
  2. Uwe na Leseni ya Biashara ya Mazao ya Kilimo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.
  3. Andika Barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, S.L.P. 2182 Dodoma.
  4. Barua ionyeshe ni zao lipi unataka kusafirisha nje ya nchi, kwa kiasi gani (tani) na utapitisha kwa njia ipi. Mfano Bandari au Mpaka upi.
  5. KWA MTEJA AMBAYE ANAOMBA KWA MARA YA PILI
  6. Mwombaji lazima awe na TIN No.
  7. Leseni ya Mazao ya Biashara.
  8. Barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, S.L.P. 2182.
  9. Barua ionyeshe ni zao lipi anataka kusafirisha nje ya nchi, kwa kiasi gani (tani) na atapitisha kwa njia ipi. Mfano Bandari au Mpaka upi.
  10. Ripoti ya kibali alichopewa mara ya wisho (ikimaanisha utekelezaji wake hivyo hutapewa kibali kingine kama haujaleta ripoti, pia ambatisha nakala ya kibali cha awali)
  11. SIMU OFISINI: 022 – 2865951 – E-mail: dnfs@kilimo.go.tz
  12. BARUA ZA VIBALI VYA KUSAFIRISHA CHAKULA NJE YA NCHI ZINAPOKELEWA CHUMBA NA.11 JENGO LA KILIMO I