Skip to main content
Habari na Matukio

BASHE AAGIZA ZAO LA CHAI KUONGEZA AJIRA/PATO LA TAIFA

Waziri wa Kilimo, Mh. Hussein Mohammed  Bashe jijini Dodoma amekutana na Uongozi wa Umoja wa Wazalishaji Chai Tanzania(TAT) na kujadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha zao hilo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania, Mary Kipeja pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Kilimo.

Katika mazungumzo yake Waziri Bashe ameutaka umoja huo kuhakikisha unaendelea kuimarisha kilimo cha chai ili kiendelee kuzalisha ajira zaidi kwa watanzania na kuongeza kiwango cha uuzwaji wa zao hilo nje ya nchi.