Skip to main content
Habari na Matukio

Benki zatakiwa kuwakopesha wanunuzi na wasindikaji wa mazao ya kilimo

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa  Charles Tizeba  amezitaka Benki zikiwemo Benki ya Kilimo,CRDB,na NMB kuwakopesha wanunuzi wa mazao ya kilimo, wasindikaji, na wakulima wenyewe kwa kuwa wanategemeana

Akiongea kwenye  Kituo cha Taifa cha Matangazo cha TBC -1 wakati wa kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku ya Alhamisi amesema mkulima ana wadau muhimu wanaomzunguka ambao wakipata mikopo wanaweza kukifanya kilimo kiwe na  tija zaidi.

Wanunuzi wa mazao ya kilimo na wasindikiaji wa mazao hayo wana nafasi kubwa katika kuongeza soko la mkulima wa Tanzania alisema Mheshimiwa Charles Tizeba  .

Aidha amepongeza Taasisi hizo za CRDB na NMB kwa namna walivyoweza kuwakopesha wakulima  katika misimu ya kilimo iliyopita na kuwataka wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kukopeshaka.

Amewataka wakulima kusindika mazao yao kabla ya kuyauza ili waweze kufaidika na kuwa chanzo cha wazalishaji wa mali ghafi za viwandani hapa nchini.