Skip to main content
Habari na Matukio
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bibi Sophia Kaduma kuwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bib Sophia Kaduma kuwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Bib Kaduma anachukua nafasi  ilioachwa wazi na Bw. Mohamedi Muya ambaye amestaafu mwaka huu  kwa mujibu wa sheria.

 Aidha Mama Kaduma ni mzoefu katika wizara hii kwani amefanya kazi kwa muda mrefu kama Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa chakula na pia Naibu Katibu Mkuu.

Baadhi watumishi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa nyakati tofauti wameupongeza uteuzi huo kutokana na uzoefu wake.

Mama Kaduma ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 ndani ya wizara hii akianzia kama afisa wa kawaida,  alishika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Pamoja na uteuzi wa Mama Kaduma Rais Kikwete ameteua Maktibu wakuu wapya 11 na Naibu Makatibu 14.