Skip to main content
Habari na Matukio

BODI ZA MAZAO KUUNGANISHWA ILI KUUNDA MAMLAKA TATU ZA MAZAO YA KIMKAKATI - WAZIRI HASUNGA

Serikali imedhamiria kuziunganisha Bodi sita za mazao zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo na kuwa na Bodi tatu ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji

 

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo jana (tarehe 13 Disemba 2019) wakati akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Ushirika wilayani Tandahimba akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara.

 

 “Bodi nyingi lakini matokeo hayaakisi malengo ya kuanzishwa kwake kutokana na kuwa na tija ndogo hivyo Serikali imeazimia Bodi hizo zitaunganishwa” Alisema Waziri Hasunga.

 

Bodi saba zitakazounganishwa na kuunda Mamlaka moja ya Kusimamia Mazao ya Kimkakati ni pamoja na Bodi za Kahawa, Pamba, Mkonge, Tumbaku, Pareto, Chai, Korosho na kuongezea mazao ya Alizeti na Chikichi.

 

Mamlaka nyingine itasimamia mazao ya nafaka, mboga mboga na matunda (Cereal and Horticulture Authority).

 

Aidha, Waziri wa Kilimo amesema kuwa Wizara ipo katika mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ushirika pamoja na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika - COASCO ili kuimarisha Sheria na kuwa na usimamizi madhubuti wa tasni ya Ushirika nchini.