DIAMOND ATEMBELEA KITUO CHA VIJANA WA BBT BIHAWANA
Mwanamuziki, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz leo Mei 19, 2023 ametembelea kituo atamizi cha kilimo cha Vijana wa programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) cha Bihawana jijini Dodoma.
Diamond aliwapongeza vijana hao na kuwasihi kufanya kazi kwa bidii kwsni kilimo kinaweza kuwatengenezea utajiri mkubwa hapo baadae.
"Najua hapa ni mahali ambapo mnaweza kujitengenezea mafanikio yenu ya muda mrefu na kama mkijikita kwenye kilimo hiki sawasawa baada ya miaka kadhaa mtapata utajiri, mimi nimeona fursa kwenye kilimo" amesema Diamond.
Awali Diamond alipokuwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Waziri Bashe alimualika kutembelea miradi mikubwa ya kilimo inayoendelea mkoani Dodoma kwa lengo la kujionea uwekezaji unaofanywa na Wizara ya Kilimo kwenye kuikuza na kuboresha sekta hiyo.