Skip to main content
Habari na Matukio

GHALA LA NAFAKA ITILIMA-SIMIYU KUWEKWA CHINI YA USIMAMIZI WA WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA(NFRA)

GHALA LA NAFAKA ITILIMA-SIMIYU KUWEKWA CHINI YA USIMAMIZI WA WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA(NFRA)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim M. Majaliwa leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ghala la nafaka katika Kijiji cha Ikindilo,Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu na kuitaka Wizara ya Kilimo kuhakikisha inasimamia kikamilifu uendeshaji wa ghala hilo lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1500*za nafaka ili lilete manufaa kwa wakulima wa Wilaya ya Itilima ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

Katika hatua nyingine Mh Waziri Mkuu Majaliwa amepokea  maombi kutoka kwa wabunge wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga juu ya usimamizi wa ghala hilo la nafaka kuwa chini ya NFRA ili kuongeza ufanisi.

Akiulezea manufaa ya mradi huo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavundeamesema mradi huo wa ujenzi wa ghala unalenga kwenye udhibiti wa sumukuvu na kuzuia upotevu wa mazao baada ya mavuno kwa kuhusisha ujenzi wa ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1500 za nafaka,maabara,sehemu ya kukaushia nafaka na vifaa vya kisasa vya maabara.

“Kwanza kabisa napenda kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na usaidizi wako Mheshimiwa Waziri mkuu kwa kazi kubwa inayofanyika katika Sekta ya Kilimo.Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa maelekezo ambayo umenipatia hapa naomba niutamkie umma wa wananchi wa Itilima ya kwamba Ghala hili ambalo lipo chini ya Halmashauri tutawakabidhi pia Wakala wa Uhifadhi wa Chakula Tanzania (NFRA) kwa ajili ya uendeshaji wake ili kuongeza ufanisi”Alisema Mavunde

Naye Mbunge wa Jimbo la Itilima Mh.Njalu Silangaameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya kilimo,afya,elimu na miundombinu katika jimbo lake na kuahidi kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya watahakikisha miradi yote inajengwa kwa kiwango cha kuridhisha na thamani ya fedha inaonekana.
Mh.Waziri Mkuu Majaliwa yupo kwenye ziara ya siku tatu mkoani Simiyu kwa ajili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi