Skip to main content
Habari na Matukio

Kamati ya Zabuni ya Uagizaji Mbolea kwa Pamoja Yakutana

Kamati ya zabuni ya uagizaji mbolea wa pamoja imekutana hivi karibuni katika ukumbi wa Mifugo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi lengo likiwa ni kufungua maombi ya awali ya makampuni yaliomba kununua na kusambaza pembejeo hiyo kwa wakulima.

Akizungumza baada ya mkutano mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Bwana Lazaro Kitandu alisema jumla ya waombaji wa zabuni walikuwa  20 na waliorudisha zabuni hizo ni  17 sawa na 85% ambazo kamati ilizifungua kwa hatua ya awali.

“Mchakato huo unafanyika kwa uwazi ambapo washindi wa hatua ya wali watatakikiwa kuleta makadirio ya bei za kusambaza mbolea hizo kwa wakulima kwa mwaka 2017/18 ambapo sheria inamtaka mzabuni mwenye gharama ndogo kupewa kipaumbele” alisema bwana Kitandu

Aidha mbolea zitakazo angizwa zitakuwa ni aina ya Urea na DAP ambazo ni maalum kwa kupandia na kukuzia mazao, mfumo  huu wa uagizaji unaruhusu mtu yeyote mwenye sifa kuagiza mbolea hiyo kwa utaratibu uliowekwa alisisitiza bwana  Kitandu.

Hata hivyo Bwana Kitandu aliongeza kuwa  mfumo huu wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja utasaidia upatikanaji kwa wingi na kwa bei ndogo kutokana na ushindani utakao kuwepo baina ya makampuni.

Hata hivyo kitandu aliwataka wakulima kuwa waangalifu wanaponunua mbolea za kupima kwakuwa nyingi zimekuwa na viwango  vidogo kutokana na namna zinavyo hifadhiwa,pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo kwa namna bora ya matumizi ya mbolea katika shamba.

Awali utaratibu wa uagizaji wa mbolea, makampuni yalikuwa yanajipangia bei hivyo mbolea kuwa na bei kubwa ifikapo kwa mkulima tofautai na mfumo huu ambao TFRA pamoja na majukumu mengine  watawasiliana na makampuni ya yanayozalisha mbolea ndani na nje ya nchi ili kuepusha udanganyifu wa gharama za ununuzi zinzosababisha mkulima kupata mbolea kwa bei kubwa. Alisema bwana Kitandu