Skip to main content
Habari na Matukio

KATIBU MKUU KILIMO KUSAYA AGAWA PIKIPIKI 18 KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amesema kuwa serikali imeendelea kuboresha sekta ya kilimo kwa kutoa Dola Milioni 35.3 kwa ajili ya kuwezesha mapambano dhidi ya Sumukuvu katika mazao ya wakulima nchini.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma wakati wa kutoa pikipiki kwa wakurugenzi wa halmashauri 18 wa Tanzania bara kwa kupitia  Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC).

Kusaya amesema kuwa sumukuvu ni sumu inayotokana na kutofata  hatua sahihi katika upatikanaji wa mbegu, upandaji, upaliliaji, uvunaji na wakati wa kuhuifadhi mazao hayo pale baada ya mavuno.

Aidha Kusaya amesema utafiti unaonyesha mazao ya karanga na mahindi ndio yanayoshambuliwa sana na sumukuvi hapa nchini.

“Hivyo  serikali kulinda usalama wa wananchi wake tumepanga kujenga maabara kuu ya mazao itakayokuwa inaangalia ubora wa mazao yote yatakayo kuwa yanazalishwa hapa nchini ili kuimarisha usalama wa mazao na vile vile kulinda uchumi wa taifa pamoja na maisha ya watanzania kwa ujumla”, ameweka wazi Kusaya.

Kusaya ameendelea kusema kuwa Kibaha watakuwa na Karantini itakayokuwa na mbengu mbali mbali na mafunzo mbali mbali ya kilimo yatafanyika pale ili kuboresha usalama wa mazao nchini kwa kuhakikisha nchi ina zalisha mazao salama yatakayo wezakuuzwa nje ya nchi na ndani ya nchi.

Pia amesema kuwa watajenga kituo cha umahiri wilayani Kongwa  kitakacho kuwa ni sehemu muhimu katika sekta ya kilimo kwa kutoa taaluma mbalimbali za kilimo.

Katika Mradi wa TANIPAC  halmashauri 12 watajenga maghala  12 na mawili visiwani Zanzibar  kwa lengo la kusaidia wakulima pale wakisha lima na kuvuna  basi mazao hayo yatahifadhiwa katika maghala hayo chini ya usimamizi wa  wataalamu wa kilimo ili kuweza kuhakikisha usalama wa mazao hayo unapatikana kwa asilimia zote.

Kusaya amesema kuwa serikali kupitia wataalamu wake wataendelea kutoa elimu kwa watanzania ili kuleta uelewa kwa jamii juu ya kuhifadhi mazao yao kwa ufasaha kwa lengo la kuongeza tika katika sekta ya kilimo.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu TAMISEMI , Mkuurugenzi wa Sekta za Uchumi na Uzalishaji TAMISEMI, Leo  Martin amesema kuwa wakurugenzi katika mamlaka za serikali za mitaa wamekabidhiwa pikipiki hizo kama vitendea kazi hivyo ziwezeshe kufanya shughuli sahihi katika maeneo yao kwa manufaa ya watanzania wanao waongoza.

Naye Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC) amesma sasa ni wakati sahihi wa wakurugenzi katika maeneo yao kuwa na elewa ju ya swala la sumukuvu kwa jamii yao na ili kufanyikisha hilo lazima wananchi wao kufanya hatua sahihi katika kilimo chao ili kufikia malengo ya uzalishaji wao na kuwa salama katika chakula wanachokula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akitoa neon la shukrani kwa niaba ya wakurugenzi wenzake  ametoa rai kuwa na ushirikiano wa karibu katika vita dhidi ya sumukuvu hapa inchi ili taifa kwa ujumla kuweza kufikia malengo ya kuwa na usalama katika mazao yanayozalishwa hapa nchini.