Skip to main content
Habari na Matukio

KATIBU MKUU KUSAYA AITAKA TAHA NA WIZARA YA KILIMO KUWA NA TAKWIMU ZINAZOFANANA.

Katibu Mkuu Kilimo ameeleza kuwa Wizara ina takwimu tofauti na  Taasisi inayijishughulisha na  kilimo cha mbogamboga na matunda (TAHA ) hivyo amewaagiza wataalam kufanya kazi  kwa ukaribu ili kuwe na takwimu sahihi. Kwa kufanya hivyo itasaidia kupata takwimu ya nchi kwa upande kilimo cha mbogamboga.

Kusaya alizungumza hayo mara baada ya kuitembelea Taasisi hiyo na kupata maelezo mafupi kuhusiana na shughuli wanazofanya na changamoto zinazowakabili.

Hata hivyo Kusaya ameeleza  jinsi  Wizara inavyoithamini TAHA na kuona ni vyama kuifahamu kiundani shughuli wanazofanya na changamoto zilizopo ili kuweza kuzitatua. Aidha Kusaya ameeleza jitihada zinazofanywa na Wizara katika kuhakikisha sekta hii inafanikiwa zaidi.

Katika maelezo yake Katibu Mkuu Kusaya amegusia Sheria ya Afya ya mimea ya mwaka 2020 ambapo itaanzisha mamlaka ya viuatilifu vya  afya ya mimea  na   kusaidia kupata elimu kwa kushirikiana na wakulima.

Aidha,Kusaya amesema kwamba Wizara kwa kushirikiana na TAHA imefanya tathimini ya maabara 3 ambazo ni SUA, Arusha TPRI na PHS.Maabara hizi zikipata ithibati zitawasaidia wakulima na Serikali kiujumla.