Skip to main content
Habari na Matukio

KATIBU MKUU MHE. KUSAYA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA WIZARA YA KILIMO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo  Mhe. Gerald  Musabila Kusaya leo tarehe 9/03/2020 amekutana na Menejimenti ya Wizara ya Kilimo katika Ukumbi wa mikutano wa Wizara uliopo Mtumba ili kuweza kufahamiana na kujua majukumu yanayotekelezwa kwa kila Idara na Vitengo vya Wizara.

 Kusaya amefanya mazungumzo hayo mara baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli  kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambapo amechukua nafasi ya Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye  atapangiwa kazi nyingine katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kabla ya uteuzi huo Bw.Kusaya alikuwa Mwenyekiti wa Timu Maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kuchunguza masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la mkonge Mkoani Tanga.

Aidha, katika kikao hicho Mhe. Kusaya ametoa maagizo kuwa aandaliwe  kikao cha wiki moja ili kila Idara na Vitengo wapate muda wa kueleza kiurefu majukumu yao wanayotekeleza na kuwasilisha kwake hard copy na soft copy ya taarifa hiyo. Pia amesema  Wakuu wa Idara na Vitengo wanatakiwa kuhudhuria na maafisa wote walio chini yao.