Skip to main content
Habari na Matukio

KATIBU MKUU MWELI AMTEMBEZA DIAMOND KWENYE SHAMBA LA CHINANGALI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli  amemtembeza Mwanamuziki Diamond Platinumz  kwenye shamba la Chinangali wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Mweli aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kilimo, Mhandisi Juma Mdeke ambaye alimueleza Diamond hatua zote za kitaalamu zilizofuatwa katika maandalizi ya shamba hilo.

Shamba la Chinangali ni miongoni mwa mashamba yanayoandaliwa kwa ajili ya Vijana wa programu ya Building a Better Tomorrow (BBT).

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe alimualika Diamond kutembelea miradi mikubwa ya Kilimo inayotekelezwa mkoani Dodoma.