Skip to main content
Habari na Matukio

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo akutana na Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe leo amefungua mkutano wa kikazi wenye lengo la kubadilishana uzoefu na kujenga uwezo kati ya Wakala waTaifa wa HifadhiyaChakula (NFRA) Tanzania Bara na WizarayaKilimo Maliasili Mifugona Mazingira.

Akimkaribisha, KatibuMkuu, KaimuMtendajiMkuu wa Wakala wa Taifawa Hifadhi ya Chakula amesema kwakipindi kirefu SerikaliyaMapinduzi ya Zanzibar kupitiaWizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugona Uvuvi imekuwa  haina Wakala waTaifa wa  Hifadhi ya  Chakula    kama ilivyokuwa NFRA Tanzania Bara na ndiyo  maana   ugeni huou mekuja Dodoma kwa  ajili ya kujifunza.

Akifungua  Mkutano huo, Eng. Mtigumwe amesema  kuwa suala la akiba ya chakula nijambojema na kuongeza kuwa nijukumu la Serikali kuhakikisha akiba ya chakula inakuwepo na kwamba upande wa Tanzania Bara, Serikali imekuwa ikitenga bajeti kila mwaka kwaajili ya kununua nafaka (Mahindi)  kwa lengo la kusaidia wananchi wakati wa uhitaji.

Eng.Mtigumwe ameongeza kuwa ninafasi nzuri kwa kila upande kujifunza kutoka kwa mwenzake hasa kwa kuzingatia kuwa asili ya watu wakila upande wana aina ya chakula wanachokipenda na kuongeza kuwa Tanzania Bara mahindi ndiyo kipaumbele wakati Tanzania Visiwani mchele ndiyo kipaumbele.

Mkutano huo wakikazi utakuwa wa siku moja na baadae ujumbe kutoka Zanzibar utapata nafasi ya kutembelea maghala ya Wakala wa Taifa Kanda ya Makambako.