Skip to main content
Habari na Matukio

KM Apokea Vitabu vya ASDP II Kutoka Bill and Melinda Gates na USAD

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo  Eng. Mathew Mtigumwe  amepokea jumla ya vitabu na majarida 1600 kutoka kwa  mshauri mwelekezi wa  mfuko wa Bill and Melinda Gates  foundation Professor  Marcelina  Chijoriga walipokutana ofsini kwake hivi karibuni

Akiongea na KM Professor Chijoriga amesema kuwa taasis ya  Bill and Melinda Gate imegawa vitabu vikubwa vya kingereza 500, vitabu vidogo vya kiswahili 400  vitabu vidogo vya kingereza 100 na vipeperushi 900  ili viweze kutumika wakati wa  uzinduzi wa mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili ASDP II.

Naye KM ameishukuru taasis hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa michango yao kwa lengo la  kuendeleza sekta ya kilimo

Pamoja na Bill and Melinda Gate tumepokea vitabu vingine 200 kutoka shirika la USAD lengo likiwa ni kufanikisha uzinduzi wa programu hiyo ya kuendeleza sekta kilimo wawamu ya pili utakao fanyika hivi karibuni

Aidha vitabu hivyo vinauelezea mradi  huo wa ASDP II kwa namna ambavyo utatekelezwa, vipaumbele vyake pamoja na namna ya ushirikishwaji wa sekta za kilimo na sekta binafsi