Skip to main content
Habari na Matukio

LINDI KUPATIWA MICHE YA MINAZI LAKI TANO

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema wakulima wa Mkoa wa  Lindi kupatiwa miche laki tano ya minazi Kwa ajili ya kupanda na kuanza kuvuna katika kipindi cha miaka minne ijayo. 

Waziri Bashe amesema hayo tarehe 19 Septemba 2023 akiwa katika ziara ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Lindi wakati wa mkutano wa hadhara Mitwero, Lindi. 

Amesema kuwa Wizara ya Kilimo itagawa miche hiyo mwaka huu kutokana na uhitaji mkubwa wa nazi nchini.

"Mkoa wa Lindi wakulima wanazalisha mazao makuu manne makubwa yakiwa ni korosho, mbaazi, ufuta na mnazi.  Hivyo, Wizara ya Kilimo itawagaia wakulima wa Lindi miche laki tano kufuatia utafiti wa kina uliofanywa kwa miche ijulikanayo kama East African Tall ambayo inavunwa kuanzia miaka minne baada ya kupandwa,” amesema Mhe. Waziri Bashe.

Serikali ina matumaini kuwa wakulima wa minazi watafaidika kwa haraka na miche hiyo na kuongeza wingi wa nazi ili kukidhi hitajio lake kwa jamii.