MAADHIMISHO HAYA YASAIDIE WANANCHI KUPATA MBEGU BORA ZA KILIMO -RC.SINGIDA
Na.Beatrice Kimwaga
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi wafike kwa wingi kwenye maonesho haya ya Siku ya Chakula Duniani ili waweze kupata ushauri,utaalam na mambo mbalimbali kama vile matumizi ya mbegu bora na za muda mfupi ambazo ni rafiki kwa mazingira ya mkoani hapo hasa katika msimu huu wa Kilimo.
Mhe.Nchimbi aliyasema hayo mara tu alipowasili katika viwanja vya Bombadier baada ya kukutana na timu ya Uratibu ambapo alitoa maagizo hayo. Hata hivyo Mhe.Nchimbi aliridhishwa na teknolojia zinazotolewa na wataalam wa Kilimo waliopo katika viwanja hivyo.
Aidha, amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga kwa kuchagua Mkoa wake kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo yalioanza tarehe 10 Oktoba ambayo yanatarajiwa kufikia kilele chake tarehe 16 Oktoba,2019.