Skip to main content
Habari na Matukio

Mashamba Darasa Kutumika Kuwabadilisha Wakulima Mkoani Mororgoro

Wakulima Mkoani Morogoro wametakiwa kutembelea mashamba darasa na kuwafuata maafisa ugani ili kujifunza namana bora ya uzalishaji wa mazao hasa mpunga.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Uzalishaji Bwana Charles Levi wakati wa sherrehe za siku ya mkulima iliyofanyika  Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Mkindo amesema wakulima ambao hawajapata mafunzo wanatakiwa kutembelea mashamba darasa na kuomba ushauri kwa wataalamu wa kilimo walio karibu nao ili kuboresha mbinu zao za uzalishaji katika kilimo

Aidha Bwana Levi amesema kuwa wameanzisha mashamba darasa katika Wilaya zote Mkoani Morogoro kwa lengo la kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu bora za kilimo na mbinu za kisasa za uzalishaji

 Bwana Levi ameeleza kwamba katika mashamba darasa hayo  Wakala wa Uzalishaji wa Mbegu (ASA) walitoa aina mbalimbali za mbegu zikiwemo TXD 306, Nerica 1,Nerika 4,Nerika 7,komboka, supa na Mwangaza ambapo wakulima hutakiwa kuchagua aina moja au mbili za mbegu ambazo wamezipenda.

Hata hivyo Wilaya ya Mvomero wakulima wengi wamechagua  mbegu aina ya Komboka Saro pamoja na Supa kutokana na uzaaji,upachaji na ustahimilivu wa  ukame zilizo nazo’ alisema Bwana Levi

Aidha Wakala imejipanga kuwatumia mabwanashamba, vyombo vya habari na wakulima viongozi katika kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu bora pamoja na mbinu za kisasa za uzalishaji.

Katika kuimarisha Zoezi la usambazaji wa mbegu wakala Kupitia taasisi na wataalam mbalimbali tumefanya  tafiti ili kubaini mahitaji halisi na kalenda za kilimo kwa kila eneo ili kuweza kusambaza mbegu hizo kwa wakati, alisisitiza Bwana Levi

Halima Hamisi ni Mkulima wa Kikundi cha Ushauri anasema ASA wamewasadia kupata mbegu bora kama Komboka na Mwangaza ambazo hizo ndizo tunazitegemea sana kutuondoa katika umaskini kwa kuwa  zinzaa sana zinahimili ukame na zinakomaa mapema

Kutokana na elimu niliyopata  nategemea msimu wa kilimo unaokuja nitalima shamba langu mwenyewe na nitayatumia mafunzo haya kuhakikisha najikwamua na umaskini, alisema Halima