Skip to main content
Habari na Matukio

MHE BASHUNGWA AWASHAURI WANAUME KULA VYAKULA VYENYE VIUNGO (SPICES)

Moja kati ya matatizo yanayowakumba watu wengi kwa kizazi cha sasa ni tatizo la magonjwa mbalimbali ikiwemo uzito, tatizo hili limekuwa chanzo cha matatizo mengine makubwa na yenye madhara makubwa kwa afya ambayo wakati mwingine husababisha kifo.

Magonjwa ya moyo, kisukari, shinikio la damu la kupanda na kushuka, matatizo ya figo na viungo vingine vya mwili pamoja na kukosa mvuto wa kawaida yanasabishwa na mtu kuwa na uzito ambao anashindwa kuumudu.

Njia pekee ya kukabiliana na kadhia ya magonjwa mbalimbali mwilini hususani kwa wanaume ni kula vyakula vyenye viungo mbalimbali (Spices) kwani zina faida nyingi kwenye afya ya wanaume.

Ushauri huo umetolewa tarehe 6 Februari 2019 na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma.

Madhara ya kutokula vyakula vyenye viungo kwa wanaume husababisha uzito kuongezeka kutokana na mtindo fulani wa maisha ya mwanadamu na pia unaweza kupungua kutokana na mtindo huu huu wa maisha ambao kama ukimudu kuuzingatia hasa kwenye chakula unaweza kupungua uzito na kuishi maisha salama.

Mhe Bashungwa alisisitiza kuwa kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wanaume kuugua magonjwa mbalimbali huku akibainisha kuwa tatizo linalopelekea kadhia hiyo ni kutokula vyakula vyenye viungo mbalimbali.