Skip to main content
Habari na Matukio

Mhe. Hassunga abainisha Mafanikio na Changamoto zinazoikabili Wizara ya Kilimo

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga leo amwapongeza Wakuu wa Taasisi na Bodi za Mazao zilizo chini ya wizara kwa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya wizara kwa msimu wa mwaka 2019/20.
Waziri Hasunga amesema wizara yake katika mwaka 2018/2019 imepata mafanikio mbalimbali yakiwemo kuanzisha mfumo wa kielectoniki wa kusajili wakulima nchini ili kujua idadi,aina ya zao,
Aliendeakusema kwamba Wizara imefanikiwa kurejesha kinu kikubwa cha usagishaji nafaka kilichokuwa kimebinafsishwa kwa kampuni Binafsi ya Mkoani Arusha ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa sasa inasimamia kiwanda hiki pamoja na kile cha Iringa ili vitumike kuzalisha bidhaa za nafaka kwa kiwango cha kimataifa.
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya Chakula kwa asilimia 103 na kuifanya nchi kujitosheleza kwa chakula."Tanzania ina usalama wa chakula kwa asilimia 119 na kufanya iongoze kati ya mataifa ya Afrika Mashariki." Waziri alieleza
Hata hivyo Waziri amebainisha Changamoto zinazotatiza Wizara kwa sasa kuwa ni baadhi ya watendaji wa wizara,taasisi na Bodi za Mazao wanatuhumiwa kwa vitendo vya rushwa.
"Hii inachafua taswira nzuri ya wizara ,hivyo naagiza Katibu Mkuu uchukue hatua za haraka za kinidhamu." Aliagiza waziri
Kikao kazi hiki ni cha tatu kufanyika tangu Waziri Hasunga ateuliwe na Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuongoza wizara ya kilimo nchin