Skip to main content
Habari na Matukio

Mkakati wa Kujitosheleza kwa Mafuta ya Kupikia hapa Nchini

katika kuhakikisha uzalishaji  wa mafuta unaongezeka hapa nchini, wakulima wametakiwa kuendelea kulima alizeti aina ya 'record' kwa kuwa aina hiyo ina uwezo mkubwa wa kuzaa na kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa,magonjwa na ukame .

kwa kipindi kirefu  watanzania wamekuwa wakitumia mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi na kiasi kidogo sana kutoka hapa nchini kwa sababu tu nchi ilikuwa haijitoshelezi kwa bidhaa hiyo.

Pamoja na kwamba tanzania ina idadi kubwa ya michikichi, minazi, alizeti pamoja na mazao mengine yanayofaa  kuzalisha mafuta ya kupikia lakini kwa sababu moja au nyingine haiwezi kuzalisha kiasi toshelevu.

Ni kwa sababu hiyo sasa serikali ikaamua kupeleka teknolojiapamoja na elimu kwa wakulima lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya mafuta.

Uzalishaji wa alizeti  umekuwa ukiongezeka kila mwaka kutokana na muitikio wa wakulima, kwa mfano  mwaka 2008 uzalishaji wa alizeti ulikuwa tani 500,000 lakini kufikia mwaka 2015 uzalishaji wa zao hilo umefikia tani 3,000,000.

Takwimu zinaonesha kuwa ongezeko hilo limesababishwa na mambo mengi ikiwemo mkono wa serikali katika kuhakikisha  mbegu bora za alizeti zinapatikana kwa urahisi ikiwemo 'record'. .

Kaimu mtendaji mkuu wa Wakala wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mbegu bora za Kilimo Dkt Sofia Kashenje  alibainisha kuwa, mbegu ya 'record' pamoja na kwamba iligunduliwa miaka zaidi 40 iliyopita lakini bado imekuwa ikifanya vizuri kwa uzalishaji na utoaji wa mafuta.

Kwa mujibu wa Dkt. Sofia,  aina hii ya mbegu ya 'record' ilipogunduliwa ilikuwa  inatoa magunia 10 hadi 15 kwa ekari na  mafuta kwa asilimia 48 , hata hivyo, pamoja na ukale huo bado imeendelea kufanya vizuri kwani ikilimwa kwa kufuata utaratibu mzuri ina uwezo wa kutoa magunia 12 na  mafuta kwa asilimia 32.

Hata hivyo, kwa mwaka 2016/17 wakaguzi wa mbegu za kilimo Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI), katika taarifa yao ya ukaguzi wa mbegu za alizeti mashambani, imeonesha kuwa asilimia 90 ya  makampuni yanayozalisha alizeti hapa nchini yaalikuwa yaamelima aina ya 'record', hii ni dalili kwamba bado aina hii ya alizeti ina matokea mazuri alisistiza Dkt. Sofia

Aidha, Dkt Sofia aliendelea kusema kuwa, zipo aina zaidi ya 15 za mbegu za alizeti ambazo zimeingizwa kutoka nje na wafanya biashara wa tasnia ya mbegu na wakulima wamekuwa wakizitumia  lakini wengi wamekiri kwamba aina ya 'record' ni bora zaidi hasa kama mbugu haitarudiwa kulimwa.katika kuhakikisha uzalishaji  wa mafuta unaongezeka hapa nchini, wakulima wametakiwa kuendelea kulima alizeti aina ya 'record' kwa kuwa aina hiyo ina uwezo mkubwa wa kuzaa na kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa,magonjwa na ukame .

kwa kipindi kirefu  watanzania wamekuwa wakitumia mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi na kiasi kidogo sana kutoka hapa nchini kwa sababu tu nchi ilikuwa haijitoshelezi kwa bidhaa hiyo.

Pamoja na kwamba tanzania ina idadi kubwa ya michikichi, minazi, alizeti pamoja na mazao mengine yanayofaa  kuzalisha mafuta ya kupikia lakini kwa sababu moja au nyingine haiwezi kuzalisha kiasi toshelevu.

Ni kwa sababu hiyo sasa serikali ikaamua kupeleka teknolojiapamoja na elimu kwa wakulima lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya mafuta.

Uzalishaji wa alizeti  umekuwa ukiongezeka kila mwaka kutokana na muitikio wa wakulima, kwa mfano  mwaka 2008 uzalishaji wa alizeti ulikuwa tani 500,000 lakini kufikia mwaka 2015 uzalishaji wa zao hilo umefikia tani 3,000,000.

Takwimu zinaonesha kuwa ongezeko hilo limesababishwa na mambo mengi ikiwemo mkono wa serikali katika kuhakikisha  mbegu bora za alizeti zinapatikana kwa urahisi ikiwemo 'record'. .

Kaimu mtendaji mkuu wa Wakala wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mbegu bora za Kilimo Dkt Sofia Kashenje  alibainisha kuwa, mbegu ya 'record' pamoja na kwamba iligunduliwa miaka zaidi 40 iliyopita lakini bado imekuwa ikifanya vizuri kwa uzalishaji na utoaji wa mafuta.

Kwa mujibu wa Dkt. Sofia,  aina hii ya mbegu ya 'record' ilipogunduliwa ilikuwa  inatoa magunia 10 hadi 15 kwa ekari na  mafuta kwa asilimia 48 , hata hivyo, pamoja na ukale huo bado imeendelea kufanya vizuri kwani ikilimwa kwa kufuata utaratibu mzuri ina uwezo wa kutoa magunia 12 na  mafuta kwa asilimia 32.

Hata hivyo, kwa mwaka 2016/17 wakaguzi wa mbegu za kilimo Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI), katika taarifa yao ya ukaguzi wa mbegu za alizeti mashambani, imeonesha kuwa asilimia 90 ya  makampuni yanayozalisha alizeti hapa nchini yaalikuwa yaamelima aina ya 'record', hii ni dalili kwamba bado aina hii ya alizeti ina matokea mazuri alisistiza Dkt. Sofia

Aidha, Dkt Sofia aliendelea kusema kuwa, zipo aina zaidi ya 15 za mbegu za alizeti ambazo zimeingizwa kutoka nje na wafanya biashara wa tasnia ya mbegu na wakulima wamekuwa wakizitumia  lakini wengi wamekiri kwamba aina ya 'record' ni bora zaidi hasa kama mbugu haitarudiwa kulimwa.