Skip to main content
Habari na Matukio

Mpango Kabambe wa Mageuzi ya Kilimo wazidi kujadiliwa

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Taasisi ya African Agriculture Transformation Initiative (AATI) imekutana na Wadau wa Kilimo kupitia rasimu ya Mpango Kabambe wa Mageuzi ya Kilimo (Agriculture Transformation Master Plan) ili kufanya wasilisho hilo na kupokea ushauri, maoni na maboresho. 

Rasimu hiyo imeandaliwa na wataalamu waelekezi kutoka kampuni inayoitwa McKinsey & Company na wataalamu wa Wizara ya Kilimo.  Aidha, zoezi hilo la mapitio na ukusanyaji wa maoni ni endelevu ambapo vikao kadhaa vimeshafanyika kwa kuhusisha menejimenti ya Wizara, Sekta zilizo chini ya Wizara na Wabia wa Maendeleo. 

Mkutano huo umefanyika tarehe 2 Novemba  2023 katika Hoteli ya Best Western iliyopo jijini Dodoma.