Skip to main content
Habari na Matukio

Parachichi ya Tanzania sasa rasmi soko la Afrika Kusini

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Tanzania imepata kibali kuuza parachichi katika soko la Afrika Kusini baada ya mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 10.

Akizungumza katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleo kwa wananchi kupitia sekta ya kilimo, Bashe amesema Mamlaka ya Mazao Afrika Kusini imeidhinisha mauzo ya moja kwa moja ya parachichi inayolimwa Tanzania nchini humo.

Mbali na ukweli kwamba parachichi yetu ni bora pia msimu wetu wa mavuno unatupa fursa ya ushindani zaidi kulinganisha na parachichi zinazolimwa sehemu zingine,” amesema.

Hata hivyo, Bashe aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwa, Serikali inafanya mipango kufungua soko la parachichi nchini India.