Skip to main content
Habari na Matukio

RAIS SAMIA ARIDHISHWA NA GHALA LA KUHIFADHIA MAZAO

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 17 Septemba 2023 amezindua ghala la kuhifadhia mazao lililopo Mangaka katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara na kuridhishwa na jengo hilo lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1500 za nafaka mbalimbali.

Mhe. Rais Samia amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Mtwara iliyoanza tarehe 15 Septemba 2023 na kuwaeleza wananchi wa Masasi kuwa changamoto ya bei ya zao la korosho litatatuliwa hivi karibuni kupitia kujengwa kwa kongani la viwanda vya kubangua korosho katika maeneo ya Malanje, wilayani Nanyamba ili kuongeza thamani ya zao hilo.

"Mkoa wa Mtwara ndiyo utakuwa na kituo cha kukoboa korosho zote zinazozalishwa  hapa Mtwara na zitawekwa thamani ili ziuzwe kama korosho zilizokobolewa, lakini hii pia itatupa faida kuuza maganda ya korosho baada ya kukamua mafuta ya maganda yake,” amesema Mhe. Rais Samia.