Skip to main content
Habari na Matukio

RAIS SAMIA AWATAKA WAKULIMA WA KOROSHO KUSAFIRISHA ZAO HILO KWA VIBALI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima pamoja na wafanyabiashara wanaosafirisha zao la korosho toka mkoani Mtwara kusafirisha kwa vibali maalum hali itakayosaidia upatikanaji wa taarifa maalum kuhusiana na uzalishaji na usafirishaji wa zao hilo nchini.

Raisi Samia ameyasema hayo hii leo tarehe 15 Septemba 2023 alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake na kukusisitiza kwa wananchi kuzingatia ubora wa korosho zinazozalishwa nchini.

"Msimu wa korosho utaanza tarehe 20 Septemba 2023,  atakayesafirisha korosho awe na kibali cha Mkuu wa Mkoa, alisema Rais Samia.

"Korosho ziwekwe kwa Grade kwanzia 1, 2, 3 na zinginezo zinazohitajika Duniani", amesema Mhe. Rais Samia.

Pia Mhe. Rais Samia aliongeza kuwa "mwaka huu Mtwara imezalisha vizuri Ufuta na Mbaazi, bei zake zimekuwa nzuri sana. Natumaini kuwa na Korosho bei itakuwa hivyo hivyo na soko litakuwa zuri".