Sensa ya Kilimo Kufanya Nchi Nzima- Ruboha
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanajiandaa kufanya sensa ya kilimo nchi nzima lengo likiwa ni kukusanya taarifa mbalimbali za Kilimo.
Akiongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkurungezi Msaidizi wa Ufuatiliaji Tathimini na Takwimu Bwana Oswald Ruboha walipokutana ofisini kwake hivi karibuni amesema, sensa hiyo inategemewa kuanza mwaka ujao wa fedha ili kupata taarifa mbali mbali za kilimo.
Aidha, Wizara za Kisekta zikiwemo Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Viwanda na Biashara, na Tamisemi zitashiriki kikamilifu katika Sensa hiyo ambapo wasimamizi wakuu ni Ofisi Taifa ya Takwimu, alisema Bwana Ruboha.
Alisisitiza kwamba sensa hiyo itagharimu kiasi cha fedha za Kitanzania bilioni 11,129,742,319 ambapo umoja wa Ulaya (EU) wametoa shilingi bilioni 5.24 kwa ajili ya sensa hiyo na kiasi kilichobaki Wizara zitatakiwa kuchangia.
kwa upande mwingine Bwana Ruboha. ametoa wito kwa watumishi na wadau wote wa kilimo kutumia mfumo wa kielekitroniki wa ufuatiliaji na tathimini ambao umekwisha kamilika kwa matumizi na upatikanaji wa takwimu mbalimbali za kilimo
timu kutoka kurugeni hiyo inajipanga kutoa wasilisho kwa menejimenti na watumiaji wa twakwimu kwa namna ambavyo mfumo huo utafanya kazi alisema Bwana Ruboha.
Aidha katika mfumo huo zipo fomu ambazo zinatumika kukusanya takwimu za kila mwezi, kila robo mwaka na kila mwaka ambapo zitawasaidia wataalamu katika tafiti mbalimbali na uimarishaji wa sekta ya kilimo . alisema bwana Ruboha.
hata hiyo mfumo huo ambao utatumika kufanya ufuatiliaji na tathimini ya ASDP II umeandaliwa kwa kuweza kutoa taarifa kutoka kila Kata nchi nzima ambazo hutumika kuandaa taarifa za kila Wilaya na Mkoa ili kupata takwimu za kitaifa alisistiza Bwana Ruboha.