Skip to main content
Habari na Matukio

SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO BAINA KATI YA JAMHURI YA TANZANIA NA JAMHURI YA KENYA

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe  Februari 3 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mithika Linturi katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, Kilimo IV, jijini Dodoma.

Mawaziri hao wawili wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo kwa kubadilishana ujuzi katika tafiti za kilimo ili kuongeza upatikanaji wa chakula katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.