Skip to main content

SERIKALI KUJENGA MABWAWA MAKUBWA 13. 

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inajenga Mabwawa makubwa 13 kwa jili ya kuvuna maji kwenye kipindi cha masika ili Kukuza Kilimo cha umwagiliaji nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe mapema leo hii, akizungumza na Wananchi wa Nzengo Wilaya ya Mbarali Jijini Mbeya.

Bashe amesema wakati wa masika tuna uwezo mkubwa wa kuvuna maji na kuyatumia wakati wa kiangazi, hivyo basi Serikali itajenga Mabwawa ili kuhifadhi maji.

“katika bajeti ya mwaka huu tunajenga mabwawa makubwa 13 na Bwawa moja dogo lina ukubwa wa ‘Cubic meters’ Milioni 3 na Bwawa moja kubwa lina zaidi ya ‘Cubic meters’ Milioni 95”, Bashe alisema.

Aidha Bashe amewataka Wananchi wa eneo la Ubaluku kutunza vyanzo vya maji kwa kusogea Mita 100 pamoja na zoezi la kupanda miti.

Bashe amesema wanaanchi lazima wawe mstari wa mbele kwenye suala zima la utunzaji wa vyanzo vya maji, kwa kupanda miti kuzunguka kingo za mto huo na kusogea mita 100.

“Mnisaidie kazi moja tu, wote Wananchi wote tusogee mita 100, sheria inatutaka tusoegee mita 60, lakini sisi tusogee mita 100”, Alisema Mhe. Bashe .