Skip to main content
Habari na Matukio

SERIKALI YASISITIZA UHURU WA KUUZA PARETO NJE YA NCHI

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewahakikishia Wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya kuwa Serikali haitozuia usafirishaji wa Pareto ya Unga.

Ameyasema hayo leo akiwa kwenye Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani Mbeya.

Aidha waziri Bashe amesema Serikali imetoa kibali cha ujenzi wa viwanda viwili vya Pareto mkoani Mbeya hivyo kuwahakikishia wakulima uhakika wa soko la mazao yao.