Skip to main content
Habari na Matukio

Shirikisho la vyama vya Wakulima Afrika ya Mashariki na harakati za Mkomboa Mkulima Mdogo

Mkulima mdogo ndiye mwekezaji wa kwanza kataka maendeo ya sekta ya kilimo hivyo Serikali inaandaa sera  sheria,kanuni, na taratibu ili kuwasaidia wakulima hao pamoja na  wewekezaji wengine.

Akizungumza na viongozi pamoja na wakulima wa shirikisho la vyama vya wakulima Afrika  ya mashariki  katika ukumbi wa Kilimo I leo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Janeth Simkanga ambaye alikuwa akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvivi amesema serikali inamtambua mkulima mdogo kama mwekezaji namba moja hivyo sheria kanuni na taratibu zote juu sekta ya kilimo ni lazima ziangalie maslahi ya mkulima huyo.

Aidha amesema serikali inatambua mchango wa sekta binafsi ambayo inamhusisha  mkulima mdogo katika kukuza uchumi wa nchi  hivyo wizara imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwamba katika kuingia kwenye uchumi wa viwanda ,suala la uongezaji wa thamani katika mazao ya kilimo unapewa kipaumbele.

Mama Simkanga amelitaka shirikisho hilo kuendelea kuwapatia wakulima taarifa sahihi za masoko yenye tija katika nchi wanachama ili waweze kufikia malengo yao.

Hata hivyo wizara kupitia bajeti hii ya 2017-2018 imejipanga kuhakikisha kwamba Vyama vya ushirika na mashirikisho ya wakulima vinaimarishwa  kwa kuandaa mazingara wezeshi ya shughuli zao.

Ili kuboresha huduma Wizara imejipanga  kutumia Tehama kutoa  huduma za ugani ili kuweza kuwafikia wakulima wengi kiurahisi na kusambaza taarifa muhimu kwa wakati na kwa usahihi ,

 “shirikisho la wakulima wa Afrika ya Mashariki litumiae nafasi ilinayo kwa wakulima na  kushirikiana na serikali ili kufanikisha zoezi hilo  la matumizi ya Tehama”. alisema mama simkanga

Akielezea lengo la shirikisho la wakulima wa Afrika mashariki  Rais wa shirikisho hilo Bwana Philip Kiriro amesema kwamba Kazi  kubwa ya shirikisho  ni kutetea wakulima ndani na nje ya nchi zao ili kuweza kufaidika na sera za nchi husika

Bwana Kiriro anasema Mtandao huo upo katika nchi kumi na baadhi yao ni zile za Afrika ya masharaiki ambapo wamekuwa wakishirikiana na mashirika mbalimbali kama MVIWATA na ACT ya hapa nchini kwa lengo la kuwaletea tija wakulima

“Kwa kweli  mtandao umewajengea wakulima uwezo na  kuwaongezea mahusiano na wakulima wa nchi nyingine katika kuimarisha biashara za mazao yao”.alisema Bwana Kiriro

Akitoa shukurani kwa Kaim Katibu Mkuu kwa namna serikali ya Tanzania anaovyotoa fedha nyingi kuwasaidia wakulima wadogo hapa nchini  Bwana Kiriro amesema tangu  shirikisho hili lianzishwe mwaka 2001 wakulima wa Tanzania wamekuwa wakipata msaada mkubwa kupitia serikali yao ikiwemo kurekebisha sheria mbalimbali ambazo zinaonekana kuwa vikwazo kwa wakulima.

Naye mkuu wa kitengo cha uratibu wa misaada na mashirikiano ya kimataifa wa wizara yakilimo mifugo na uvui Bi Margareth Ndaba akichingia hoja ameitaka sekta binafs  kuwashirikisha vijana kuanzia kuzalisha mpaka kusambaza  kutokana na uwezo wao mkubwa wa kupata taarifa