Skip to main content
Habari na Matukio

SUMUKUVU; MADHARA NA NAMNA YA KUDHIBITI

SUMUKUVU; MADHARA NA NAMNA YA KUDHIBITI


SUMUKUVU ni  kemikali  zinazozalishwa  na aina za fangasi /ukungu/kuvu wanaoota kwenye punje za nafaka, mbegu za mafuta,  mikunde na mazao ya mizizi (Smith et al., 2012)
Mahindi  na unga wake na karanga  na bidhaa zake huathiriwa zaidi na sumukuvu. Mazao mengine ni korosho, muhogo, alizeti, mtama na mchele.
SUMUKUVU pia hupatikana katika bidhaa za  mifugo kama vile mayai, nyama na maziwa iwapo  watakula chakula kilichochafuliwa na  sumu
Hupatikana  katika maziwa ya mama anayenyonyesha iwapo atakula  chakula chenye sumu kuvu


Kuna SUMUKUVU  za aina nyingi kulingana na kuvu anayezalisha sumu hiyo,  mfano kwa mahindi  aflatoxin, fumonisins, and ochratoxin ndiyo za muhimu zaidi.
SUMUKUVU hazionekani kwa macho, hazina harufu, ladha wala rangi. Lakini kuvu wanaozalisha sumu kuvu wanaweza kuwa na rangi kama vile kijani, kijivu, njano chafu au machungwa.
 

*download taarifa hii hapa chini*

Pakua Faili: