Skip to main content
Habari na Matukio

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSITISHWA KWA KONGAMANO LA VIJANA KATIKA KILIMO

Dar es Salaam, 16 Machi, 2020

 

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Japhet N. Hasunga (Mb) amesitisha kongamano la vijana katika kilimo lililokuwa limepangwa kufanyika Jumanne tarehe 17 Machi 2020 katika ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Agizo hili ametolewa leo  kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali  ya kuchukua tahadhari ya mikusanyiko ya watu wengi kuepusha hatari ya kusambaa kwa maambukizo ya virusi vya Corona nchini.

 

Wizara ya Kilimo inawataarifu  wadau wote wa sekta ya kilimo na vijana waliopanga kushiriki kongamano la  kujadili fursa za kilimo,mifugo na uvuvi kwa kanda ya Dar es Salaam iliyokuwa ikihusisha mikoa ya Dar es Salaam,Pwani,Morogoro,Lindi na Mtwara kusitisha kuhudhuria kongamano hilo hadi watakapotaarifiwa baadaye.

 

” Rais  Dkt.John Pombe Magufuli ametoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhali  na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maambukizi ya Corona kwa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi isiyo ya lazima” alisema Waziri Hasunga.

 

Mheshimiwa Waziri Hasunga amewataka wakulima na vijana wote nchini kuendelea kuchukua hatua za tahadhali kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya  yaliyotolewa  ili kuthibiti maambukizo ya virusi hivi hatari vya Corona hapa nchini.

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Kilimo.

DAR ES SALAAM

Pakua Faili: