Skip to main content
Habari na Matukio
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSUDIO LA SERIKALI KUVIFUTA VYAMA VYA USHIRIKA 3,436 VISIVYOKIDHI MASHARTI

1.0 UTANGULIZI

Chama cha Ushirika ni chama kinachoanzishwa kwa hiari ya watu wenye lengo la kutatua tatizo au shughuli ya kiuchumi na kijamii inayolenga katika kuwabadilisha wananchama kiuchumi au kimaisha.  Ushirika unatokana na nia ya pamoja katika kufanya shughuli fulani. Kwa kuzingatia misingi ya ushirika, ushirika ni huru na wa wazi kuingia na kutoka kwa kadri ya uamuzi wa mwanachama kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu walizojiwekea wenyewe. Vyama vya Ushirika vinaanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya Na. 6 ya Mwaka 2013.

 

Chama cha Ushirika ni Taasisi inayotakiwa ianze na kufanya kile kilichokusudiwa kwa mujibu wa katiba ya chama na sheria ya ushirika. Hivi sasa vyama vya ushirika vimegawanyika katika makundi yafuatayo: Saccos, Amcos, Ufugaji, Malaji, Huduma, Ufugajiji nyuki, Nyumba, Madini, Viwanda, Uvuvi, Umwagiliaji, Vyama vikuu,,na vinginevyo. . 

 

2.0 Majukumu makuu ya Chama cha Ushirika ni:-

 

Kuinua hali ya maisha ya wanachama wake;

 

Kutoa huduma kwa wanachama wake zikiwemo mahitaji ya pembejeo za kilimo, kukusanya, kusindika na kutafuta masoko ya bidhaa za wanachama wake;

 

Kutoa taarifa zinazohusiana na shughuli zake kwa mujibu wa sheria na

 

Kutoa huduma kwa Vyama vya Msingi kama ilivyoainishwa kwenye Masharti ya Chama.

 

Viongozi wa Ushirika wana wajibu wa kuhakikisha kuwa Vyama vya ushirika vinatekeleza majukumu kwa uwazi, haki na usawa na kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya ushirika. Kazi ya Kiongozi ni kulinda maslahi ya Wanachama na mali zao.

 

3.0 Idadi ya vyama vya ushirika kwa sasa.

Mpaka sasa daftari la Mrajis wa Vyama vya Ushirika lina jumla ya vyama 11,149 vilivyoandikishwa.  Kati ya Vyama hivyo 3,436 havijulikani vilipo (hewa), vyama 1,250 vimesinzia na vyama 6,463 vipo hai.  Kutokana na kuwepo kwa vyama hewa katika dafatri la mrajis wa vyama vya ushirika, nilimuagiza kutangaza  kwenye gazeti la Serikali kusudio la kufuta vyama hivyo kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya ushirika. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika kifungu cha 100, chama kinaweza kikafutwa kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na hizi zifuatazo:-

 

Toka kiandikishwe hakina ofisi, havijulikani vilipo na viongozi wake hawafahamiki na hawapatikani;
Vyama hivyo vimeshindwa kutekeleza takwa la kisheria  la kutayarisha makisio ya mapato na matumizi  na kuyapeleka kwa mrajisi kuyapitisha, kutayarisha taarifa ya mwaka, kufunga mahesabu na kuyapeleka  COASCO  kwa ukaguzi, kutofanya mikutano ya mwaka ya wanachama wote na bodi zao, n.k;

 

 Chama kushindwa kufanya shughuli zake ndani ya miezi sita tangu kiandikishwe;

 

 Idadi ya wanachama kupungua kwa mujibu wa mahitaji ya kisheria;

 

kushindwa  kutekeleza matakwa ya kisheria kama vile sheria za fedha za Benki Kuu ya Tanzania kwa upande wa SACCOS;

 

Maagizo kwa mrajisi wa vyama vya ushirika

 

Kwa kuzingatia matakwa ya sheria No. 6 ya mwaka 2013, ya vyama vya ushirika kifungu 100 na kanuni ya 26 Mrajisi wa vyama vya ushirika anatakiwa kutoa notisi ya kusudio la kutaka kufuta vyama vya ushirika kwenye gazeti la serikali kwa muda siku 90. Hivyo ninamuagiza mrajisi wa vyama vya ushirika kutangaza mara moja kusudio la kufuta vyama 3,436 ambavyo havitekelezi majukuu yake ya msingi na havipatikani/havijulikani vilipo. Vyama hivi vimetapakaa kwenye Mikoa yote Tanzania Bara. Asilimia kubwa ya vyama vya ushirika vilinavyokusudiwa kufutwa ni vyama vya  ushirika wa Akiba na Mikopo ambavyo ni 73.8%.  vyama hivi vingi ni matokeo ya mfumo wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ujulikanao kama (Jk fund) mpango ambao ulilenga katika kuwawezesha wananchi kiuchumi. Katika mpango huu wananchi walio wengi walianzisha SACCOS kwa lengo  la kupata mikopo  kutoka kwenye mfuko huo.  Aidha, vyama ambavyo havikupata mkopo havikuendelea na majukumu yake na hata vilivyopata mikopo baada ya kupata mikopo walitelekeza vyama vyao jambo  ambalo lilipelekea kuwa na SACCOS nyingi ambazo hazifanyi kazi.

 

(4.1) Mchanganuo wa vyama hivyo kwa misingi ya majukumu yao ni kama ifuatayvo:   

AINA YA CHAMA

IDADI YA KUFUTWA

ASILIMIA

SACCOS

2,537

73.8%

AMCOS

264

7.7%

MIFUGO

82

2.3%

VYAMA VYA WALAJI

25

0.7%

HUDUMA

72

2.1%

UFUGAJI NYUKI

17

0.4%

NYUMBA

8

0.2%

MADINI

23

0.6%

VIWANDA

102

2.9%

UVUVI

37

1.1%

UMWAGILIAJI

31

0.9%

VYAMA VIKUU

3

0.01%

VINGINEVYO

235

6.8%

JUMLA

3,436

100%

 

 

 

Orodha ya vyama vya ushirika kimkoa vinavyokusudiwa kufutwa kwenye daftari la Mrajis wa vyama.

Jedwali Na. 1: Idadi ya vyama vya Ushirika kimkoa vinavyokusudiwa kufutwa

MKOA

JUMLA YA VYAMA

ASILIMIA

MWANZA

393

11.44%

PWANI

335

9.75%

KAGERA

301

8.76%

MOROGORO

298

8.67%

ARUSHA

282

8.21%

TABORA

282

8.21%

KIGOMA

207

6.02%

MARA

151

4.39%

TANGA

136

3.96%

GEITA

119

3.46%

MANYARA

116

3.38%

IRINGA

92

2.68%

LINDI

85

2.47%

MBEYA

78

2.27%

RUKWA

70

2.04%

DODOMA

68

1.98%

SINGIDA

59

1.72%

SONGWE

54

1.57%

MTWARA

52

1.51%

KILIMANJARO

49

1.43%

NJOMBE

40

1.16%

SIMIYU

40

1.16%

DAR ES SALAAM

39

1.14%

RUVUMA

39

1.14%

SHINYANGA

34

0.99%

KATAVI

17

0.49%

JUMLA

3436

100.00%

 

Kielelezo Na.1: Asilimia ya vyama vya ushirika kimkoa vinavyokusudiwa kufutwa

 

\

Jedwali Na. 2: Orodha ya vyama vya ushirika kimkoa na aina

AINA YA CHAMA

SACCOS

AMCOS

LIVESTOCK

CONSUMER

SERVICE

BEE KEEPING

HOUSING

MINING

INDUSTRY

FISHING

IRRIGATION

UNION/JE

OTHERS

JUMLA

JUMLA KUU

2537

264

82

25

72

17

8

23

102

37

31

3

235

3436

ASILIMIA

73.84%

7.68%

2.39%

0.73%

2.10%

0.49%

0.23%

0.67%

2.97%

1.08%

0.90%

0.09%

6.84%

100.00%

ARUSHA

     205

     19

     21

     14

      5

       -

       -

      1

     13

       -

      2

       -

      2

       282

DAR ES SALAAM

      39

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         39

DODOMA

      53

      4

      1

       -

      4

      5

       -

       -

       -

       -

       -

       -

      1

         68

GEITA

     106

      2

      1

       -

       -

      4

      1

      4

       -

      1

       -

       -

       -

       119

IRINGA

      55

     20

      1

       -

      1

       -

      1

      1

      2

      3

       -

       -

      8

         92

KAGERA

     166

     11

     17

       -

     31

       -

       -

      1

      1

      2

      1

       -

     71

       301

KATAVI

      12

      1

       -

       -

      1

      1

       -

       -

       -

       -

       -

       -

      2

         17

KIGOMA

     164

     29

       -

       -

       -

       -

       -

       -

      3

      3

       -

       -

      8

       207

KILIMANJARO

         -

      1

      1

      4

       -

       -

       -

      1

      3

       -

     20

       -

     19

         49

LINDI

      85

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         85

MANYARA

      76

     23

      8

       -

       -

      3

       -

      1

      1

      1

       -

       -

      3

       116

MARA

     133

      2

      5

       -

      5

       -

      1

      4

      1

       -

       -

       -

       -

       151

MBEYA

      56

      6

      5

      1

      2

       -

       -

       -

       -

      2

       -

       -

      6

         78

MOROGORO

     230

     30

      9

      2

      1

       -

      1

      2

      1

       -

       -

      1

     21

       298

MTWARA

      52

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         52

MWANZA

     342

      5

       -

      1

     11

       -

      3

       -

      4

     10

      4

       -

     13

       393

NJOMBE

      31

      7

       -

      1

      1

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         40

PWANI

     163

     26

      2

      1

      4

       -

       -

       -

     72

     14

       -

      2

     51

       335

RUKWA

      54

      2

      2

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

     12

         70

RUVUMA

      39

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         39

SHINYANGA

      30

       -

       -

       -

       -

       -

      1

      2

       -

       -

       -

       -

      1

         34

SIMIYU

      38

      2

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         40

SINGIDA

43

7

2

0

0

1

0

4

0

1

1

0

      0

         59

SONGWE

      46

      5

      3

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

       -

         54

TABORA

     207

     55

       -

       -

      2

      3

       -

       -

       -

       -

       -

       -

     15

       282

TANGA

     112

      7

      4

      1

      4

       -

       -

      2

      1

       -

      3

       -

      2

       136

Jumla

 2,537

  264

    82

    25

    72

    17

      8

    23

  102

    37

    31

      3

  235

    3,436

           

5.0 Hitimisho

Tunavitaka vyama hivi ambavyo orodha yake itapatikana kwenye Gazeti la serikali, mtandao wa wizara ya kilimo, na mtandao wa Tume ya ushirika wajitokeze na kutoa sasabu za kwa nini wasifutwe kwenye orodha ya vyama vya ushirika. Tunavitaka vyama vyote vya ushirika nchini kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo. Vyama vyote vinatakiwa kuwahudumia wananchama wake na siyo vinginevyo. Tutaendelea kuvifuatilia kwa karibu na kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atayeendelea kukiuka maagizo na sharia hizo.

Asanteni kwa kunisikiliza.

 

Imetolewa na,

 

Japhet  N.Hasunga (Mb)

WAZIRI WA KILIMO

05 Januari,2020

DODOMA